Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiongea na
wafanyakazi wa SBL waliowakilisha katika kutoa msaada wa mifuko ya mifuko ya
saruji 500 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa wahanga wa janga la
tetemeko la ardhi lililotoa mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera mjini Bukoba mapema leo , Novemba 29,
2016.
Kampuni ya
Bia ya Serengeti (SBL) leo imetoa msaada mifuko ya saruji 500 yenye
thamani ya shilingi milioni 10 kwa wahanga wa janga la tetemeko la ardhi
lililotoa mkoani Kagera. Msaada huo ni kuitikia wito wa serikali kwa
mashirika, watu binafsi na watu wenye mapenzi mema wa kujitoa kusaidia
wahanga wa tukio hilo.
Akizungumza
katika tukio la kukabidhi msaada huo katika Ofisi ya Mkuuu wa Mkoa wa Kagera
mjini Bukoba, Meneja Usalama wa SBL, Sebastian Kalugulu aliwapa
pole wahanga wa tetemeko hilo kwa kuwahakikishia kwamba
SBL kila mara iko tayari kusaidia pindi inapohitajiwa na
jamii.
“”Tunatoa
pole ya dhati na masikitiko yetu kwa wahanga wa tetemeko la
ardhi na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka,” alisema Kalugulu,
na kuongeza kwamba SBL inaungana na watu wengine wenye mapenzi mema
kutoa msaada wa kibinadamu kwa ajili ya kuwasaidia kuhimili kadhia
iliyowapata na kurudi katika shughuli zao kawaida.
Kalugulu
alithibitisha tena kwamba kampuni hiyo ya bia imejikita katika
kuunga mkono serikali na watu binafsi wenye mapenzi mema,
mashirika na makampuni katika kuisaidia jamii katika
maeneo SBL inapoendesha shughuli zake.
“Ni
matumaini yetu kwamba msaada huu utachangia katika
michango iliyokwishatolewa na wasamaria wengine na kwamba
itawawezesha wahanga hao kujenga miundombinu
iliyoharibika na hata kuboresha maisha yao.”
Akizungumzia
mchango uliotolewa na SBL, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum
Kijuu alisema kwamba msaada huo unachangia katika
michango mingine kutoka kwa watu wenye mapenzi mema kutoka
ndani, mikoani na kimataifa ambao kmwa ukarimu waliitikia
wito wa serikali wa kusaidia.
Mkuu huyo wa
mkoa alisema kuwa atahakikisha kuwa msaada huo unaenda kwenye lengo
lililokusudiwa na kutoa wito kwa watu
zaidi kuendelea kuwasaidia wahanga.
|
No comments:
Post a Comment