Rais JPM:Atoa Agizo zito,Amwaga Tsh 10 Bilioni Gereza la Ukonga-Dar. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 30, 2016

Rais JPM:Atoa Agizo zito,Amwaga Tsh 10 Bilioni Gereza la Ukonga-Dar.

Mmoja wa askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza wakitoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli  alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Jumanne Novemba 29, 2016.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akichukua maelezo kutoka kwa  maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016.
 
Baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Rais Dkt John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Jumanne, Novemba 29, 2016. 

Askari wakiwa na shauku ya kutoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipoongea  na  maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016.

Mkuu wa gereza la Ukonga akieleza changamoto za kazi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli  alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Jumanne,Novemba 29, 2016.

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Jumanne  tarehe 29 Novemba , 2016  amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar Es Salaam  na kupiga marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.

Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi nchini na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi ya hapa nchini

Hali kadhalika Rais magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika.

''Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa nchini kuuzwa na watu binafsi hilo haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza muda wangu , amesema Rais magufuli''

Aidha Rais Magufuli ametoa shilingi 10 bilioni  kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam. 

Hatua hiyo inafuatia kilio cha askari Magereza kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi uaraiani kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi nchini na hata kuzorotesha utendaji kazi wa askari wa Jeshi hilo. 

Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia ameagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanatumika katika uzalishaji mali badala ya mfumo wa sasa ambapo baadhi ya wafungwa wamekuwa  wakitutumia rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.

 Rais Magufuli amewahakikishia Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi mengine nchini.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Jumanne Novemba 29, 2016.


PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad