Ndege Iliyobeba Wanasoka wa Brazil Yaanguka Colombia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, November 29, 2016

Ndege Iliyobeba Wanasoka wa Brazil Yaanguka Colombia.

Ndege iliyokuwa imebeba watu 72, ikiwemo timu ya soka ya klabu ya Chapecoense ya Brazil (pichani juu), imeanguka katika sehemu ya milima nchini Colombia  wakati inakaribia Mji wa Medellin.

 Maelezo kamili ya ajali hiyo hayajafahamika lakini habari zinasema kwamba kuna watu walionusurika.
Ndege hiyo ya kukodisha iliyokuwa ikitokea Bolivia, ilikuwa na timu ya  soka ambayo ilikuwa icheze katika fainali ya Kombe la Amerika ya Kusini dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya Medellin. 

 Hivyo, fainali hiyo imeahirishwa.

Ripoti zinasema ndege hiyo yenye leseni namba CP 2933, iliyoanguka muda mfupi kabla ya saa sita usiku, ilielezewa na Meya wa Medellin, Federico Gutierrez, kama “janga kubwa”, akiongeza kwamba  inawezekana kuna watu walionusurika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad