Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar umeingia kwenye jaribio jingine, baada ya Wazanzibari
40,000 kufungua kesi mahakamani kupinga uhalali wake.
Kesi hiyo
ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) na Rashid
Salum Adiy kwa niaba ya wenzake 39,999, katika Masijala ndogo ya mahakama hiyo
iliyoko jijini Dar es Salaam.
Wadaiwa
katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Adiy anasema
kuwa msingi wa kesi hiyo ni kwamba Muungano huo haukuanzishwa kisheria.
“Sisi
tunadai Muungano huu hauko kwa misingi ya kisheria na kutokana na ushahidi
tulionao, uko kisiasa tu na jambo hili linahitaji mfumo na mwenendo wa kisheria
kwa kuwa wenye mamlaka ya nchi ni wananchi,” alisema Adiy.
Alisema
kutokana na nyaraka walizonazo wanapinga hati ya Muungano inayodaiwa ilisainiwa
Aprili 22, 1964 na wanapinga uamuzi wa Baraza la Mapinduzi kuridhia Muungano
huo.
Wanapinga
barua ya Mei 6, 1964, iliyopelekwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN),
kuelezea kutambuliwa kwa Muungano huo.
Pia,
wanapinga uhalali wa barua ya Novemba 02, 1964 iliyopelekwa UN ikielezea
matumizi ya jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria iliyopitishwa na
Bunge Desemba 10, 1964 ikielezea matumizi ya jina la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Adiy na
wenzake wanadai kwa kuwa Muungano ni wa kisiasa, ndiyo maana hauwezi kuleta
manufaa kwa pande zote mbili hususani uwiano wa kiuchumi na kielimu.
Baada ya
kuwasilisha nyaraka zao wanasubiri kesi hiyo isajiliwe kwa kupewa namba katika
Mahakama hiyo na kupangiwa taratibu za usikilizwaji wake.
Mbali na
Wazanzibari 40,000, pia alisema wanayo majina mengine ambayo watayawasilisha
mahakamani baadaye, kesi itakapokuwa imeanza
|
No comments:
Post a Comment