By Peter
Elias, Mwananchi
Kampuni ya
Sumsung Afrika Mashariki (SEEA) imetangaza kuwabadilishia simu au kuwarudishia
gharama zao wateja wote walionunua simu za Samsung Galaxy Note 7 popote
Duniani.
Hatua hiyo
imefuata baada ya kubainika kwamba simu hizo ni hatari kwa sababu betri zake
zinalipuka. Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopiga marufuku uingizaji wa simu
hizo nchini kwa sababu za kiusalama.
Kwa mujibu
wa tangazo lililotolewa kwenye Vyombo vya habari, watu walionunua simu hizo
watabadilishiwa na kupewa simu ya Galaxy S7 au Galaxy S7 Edge au Galaxy Note 5
na watarudishiwa gharama za ziada.
Mbali na
kuwabadilishia simu, kampuni hiyo imefafanua kwamba wateja wanaotaka kupewa
fedha taslimu watarudishiwa fedha kamili walizonunulia Samsung Galaxy Note 7
kama wana uthibitisho wa risiti.
|
No comments:
Post a Comment