Taasisi
inayoongoza Tanzania kwa kubobea katika kutoa mikopo nafuu, Bayport Financial
Services katika kipindi cha miaka 10 iliyopita
imechangia kwa kiwango kikubwa
katika kuboresha maisha ya maelfu ya Watanzania kupitia utoaji wa mikopo.
Bayport Tanzania ni miongoni mwa taasisi tanzu
kumi za Taasisi ya Bayport Group ambayo hutoa ufumbuzi wa kifedha kwa watu binafsi walioko katika ajira rasmi
au waliojiajiri ndani ya soko linaloibukia.
Huduma zinazotolewa na taasisi
hiyo zinaboresha ujumuishwaji
kifedha kwa watu ambao hawana uwezo wa
kuzifikia huduma za kawaida za
kibenki au walio na kiasi kidogo cha
fedha katika benki.
Baada ya
kuanza shughuli zake nchini Zambia mwaka
2001, shughuli za Bayport kwa hivi sasa
zinaendeshwa katika nchi saba barani Afrika na
nchi mbili ndani ya Amerika Kusini.
Nchi hizo ni Zambia, Uganda, Ghana,
Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Msumbiji, Colombia, na Mexico.
Hivi sasa Bayport imekuwa ni msingi wa kuaminiwa na mteja ikiwa
na takribani wateja 518,000 ambao kila mara wamekuwa wakipata na hata na kufurahia huduma inazozitoa.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport
Tanzania, John Mbaga, Bayport imeshatoa
zaidi ya shilingi bilioni 48
katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015 peke yake.
Kwa upande mwingine Bayport
inachukuliwa kuwa ni ‘mlipa kodi mkubwa’
nchini Tanzania ikiwa imelipa
zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa mwaka wa fedha 2014.
“Matamanio
yetu ni kuboresha maisha ya wateja wetu
na kuwapa fursa ambazo
zitawanufaisha sio wao peke yao bali
pia watoto wao na kizazi kijacho,”
alisema Mbaga katika mazungumzo yake na
wanandishi wa habari hivi karibuni.
Aliongeza,
“Tunawasaidia kwa kuangalia unafuu utakaotokana na mtiririko wa fedha katika kipindi kifupi
ambapo matokeo yake husaidia familia
katika kuongeza na kuwa na ustawi wa kifedha
wa kudumu.”
Bayport Tanzania ilianzishwa mwaka 2006, na kwa haraka imekuwa ni
mtoaji wa mikopo kwa wafanyakazi katika sekta za umma na binafsi. Kuwepo
kwa ofisi zake 83 za kudumu na matawi 45 ya muda kumeifanya
kufika kila mkoa kwa Tanzania Bara.
Kampuni hii ina wafanyakazi wa kudumu 300 na
mtandao wa mawakala wa mauzo zaidi ya 1000.
|
No comments:
Post a Comment