“Mnyama huyo
alifariki jana,” alisema ofisa wa wanyamapori, Ashit Ranjan Paul akizungumza na
shirika la habari la AFP.
“Tumefanya
kila juhudi kumwokoa mnyama huyo ambapo maofisa zaidi ya kumi wakiwemo walinzi
wa wanyamapori, matabibu wa wanyama na polisi, tulimfuatilia na kumhudumia kwa
juhudi zote katika saa zake 48 za mwisho. Hata hivyo, ilikuwa ni bahati
mbaya,” aliendelea kusema.
Paul alisema
aliamini mnyama huyo alitokea kaskazini-mashariki mwa Jimbo la Assam nchini
India, lakini alipofika Bangladesh alicharuka na kukimbilia katika bwawa ambako
wanakijiji wa sehemu hiyo walimwokoa mnyama huyo mwenye uzito wa tani nne,
asizame.
Vyombo vya
habari vya sehemu hiyo vililaumu matibabu kwamba walimdunga mnyama huyo dawa
nyingi kupita kiasi za kutia usingizi ambazo zilimfanya awe mnyonge zaidi.
|
No comments:
Post a Comment