SIMBA SC YAANZA MSIMU MPYA WA LIGI KUU KWA POINTI 3 LEO AGOSTI 20,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 20, 2016

SIMBA SC YAANZA MSIMU MPYA WA LIGI KUU KWA POINTI 3 LEO AGOSTI 20,2016.

Mfungaji wa bao la pili la Simba SC, Fredrick Blagnon akipongezana na Laudit Mavugo.

Simba SC imeuanza vyema msimu wa ligi kuu Tanzania bara kwa kupata ushindi wa magoli 3-1 mbele ya Ndanda FC ya Mtwara katika mechi ya kwanza ya msimu wa 2016/2017 mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa taifa leo Agosti 20,2016.

Mshambuliazi mpya wa Simba SC, Laudit Mavugo alianza kuifungia klabu yake bao la kuongoza dakika ya 19 kipindi cha kwanza kabla ya bao hilo kusawazishwa na Omary Mponda dakika ya 36.

Fredrick Blagnon akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 73 kabla ya Shiza Kichuya kukamilisha ushindi kwa kukwamisha kambani bao la tatu dakika ya 79..
Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib (katikati) akipambana kuwatoka mabeki wa Ndanda FC.

Dondoo muhimu

          Mavugo na Blagnon wamefunga magoli yao ya kwanza kwenye mechi ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara.

          Goli la Mavugo ni la pili katika mechi tatu alizocheza akiwa Simba. Bao lake la kwanza lilikuwa kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, mechi ya pili ilikuwa dhidi ya URA ya Uganda ikiwa ni mechi ya pili ya kirafiki ya kimataifa.

          Salum Telela amecheza mechi yake ya kwanza kama kwenye ligi akiwa nje ya Yanga tangu alipoachana na mabingwa hao watetezi wa VPL baada ya mkataba wake kumalizika.
Golikipa wa Ndanda FC Jackson Chove akipatiwa huduma ya kwanza na madaktari wa timu hiyo baada ya kuumia wakati wa mchezo wa VPL dhidi ya Simba SC.

LIGI KUU VODACOM 2016/2017.

Jumamosi Agosti 20,2016.

Simba 3 - 1 Ndanda FC

Stand United 0 – 0  Mbao FC

Mtibwa Sugar 0 - 1 Ruvu Shooting

Azam FC v African Lyon

Majimaji FC 0 – 1  Tanzania Prisons


LIGI KUU VODACOM

Jumapili Agosti 21,2016.

Kagera Sugar v Mbeya City

Jumatano Agosti 24,2016.

Toto Afrcans v Mwadui FC

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad