Wataalamu wanasema
hakuna kiwango salama cha unywaji pombe
Utafiti mpya imedokeza
kwamba kuna uhusiano mkubwa baina ya unywaji pombe na aina saba za saratani.
Matokeo ya utafiti huo
yaliyochapishwa katika jarida la "Addiction" yanaonyesha kuna
uhusiano mkubwa wa moja kwa moja kati ya unywaji pombe na madhara ya kiafya
ingawa bado haijabainika hilo linatokea vipi kibiolojia.
Saratani ambazo
imegunduliwa zina uhusiano mkubwa na unywaji pombe ni pamoja na saratani ya
mdomo na koo, saratani ya kikoromeo, saratani ya ini, saratani ya utumbo mpana,
saratani ya matumbo na saratani ya matiti.
Mwezi Januari mwaka
huu, afisa mkuu wa matibabu nchini Uingereza alitahadharisha kwamba hakuna
kiwango chochote cha unywaji pombe ambacho hakina madhara kwa mwili.
Unywaji pombe
unakadiriwa kusababisha vifo vya watu 500,000 kutokana na saratani mwaka 2012
pekee.
|
No comments:
Post a Comment