MWENGE WA UHURU 2016:-Wawasili Ngara mkoani Kagera ukitokea Kakonko mkoani Kigoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 23, 2016

MWENGE WA UHURU 2016:-Wawasili Ngara mkoani Kagera ukitokea Kakonko mkoani Kigoma.

Wakati  Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuzindua miradi ya maendeleo yenye thamani shilingi bilioni 17,729,785,522 Mkoani Kagera na ikipokelewa katika Wilaya Ngara, Kata ya Murusagamba mpakani mwa Mkoa wa Kigoma na Kagera leo tarehe 23/07/2016…..’’.Watendaji katika Idara mbalimbali za halmasauri za wilaya wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu kwa kufuata miongozo taratibu za kazi na kutumia taaluma yao ili kuleta ufanisi na kuondoa manug’uniko katika jamii

Kauli hiyo ilitolewa na Kiongozi wa mbio za mwenge  Kitaifa George Mbijima alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa Kibondo Mkoani kigoma, wakati mwenge huo ulipofanya mbio zake wilayani Kibondo Julai 21,2016.


Mbijima ameseme kuwa hivi sasa serikali imeelekeza nguvu zake kwa Wanawake na Vijana katika kuwawezesha kwa kupitia katika halmashauri zao lakini wapo baadhi ya watendaji wasiokuwa waadilifu mara zinapotokea fursa kwa walengwa wao uzipora na kuwapa watu wao au kuziingiza katika makampuni yao binafsi

Mwenge  huo katika mbio zake wilayani Kibondo  ulitembelea miradi tisa ya maendeleo yenye thamani ya million mia 960,961,775 na kutoa elimu kwa jamii juu ya kujiepusha na matumiszi ya madawa ya kulevya , Maambukizi ya ukimwi, na kutoa hamasa kwa Vijana , Wanawake kujunga na kufanya kazi iliweze  kuongeza kipato  cha familia ambapo kiongozi huyo amewataka vijana kushiriki katika kazi na kuheshimu utu wao  waweze kuthaminiwa ndani ya jamii ndipo na shirikishwaji utakapo kuwepo

‘’Vijana kutokana na mienendo yetu mibaya tunasomeka katika jamii kuwa ni wathuni ambao hatusitahili kushirikishwa katika mambo mbalimbali ya kijamii na kifamilia lakini tukijiheshimu kwa kufuata maadili hata ushirikishwaji utakuwa na maana.''  alisema Mbijima kiongozi mbio za Mwenge 2016’’
Kwa upande wao baadhi ya Wanawake katika vikundi vyao waliotembelewa wameiomba serikali pamoja na kuweka mkazo kuwajali Wanawake na Vijana  kwa kutaka kuwawezesha walisema lakini  wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa elimu ya ujasiliamali huku vijana ambao ni Josephat Kanguye na Rodah Linus, wakipongeza uhamasishaji unaotolewa kujiepusha na madawa ya kulevya.

Katika kujibu maombi ya Wanawake hao, Mbijima ameitaka halmashauri ya wilaya ya kibondo kuhakikisha inatoa elimu kwa makundi hayo ili yaweze kufanya kazi  ipasavyo ambapo Kaimu Murugenzi wa halmashauri hiyo Said Shemahonge ameahidi baada ya wiki mbili wataanza kutoa elimu hiyo.

Habari / Picha na Muhingo Mwemezi -Kibondo/Kigoma.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad