TAZAMA PICHA 8: Rais Magufuli alivyoendelea na ziara yake Igunga na Nzega Tabora. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 31, 2016

TAZAMA PICHA 8: Rais Magufuli alivyoendelea na ziara yake Igunga na Nzega Tabora.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Jana, July 30 2016 ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoa wa Singida.

Mkoani Tabora, Rais Magufuli amezungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na amefanya mikutano ya hadhara Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.

Kuhusu kero ya maji, Dkt. Magufuli amesema Tanzania imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge
3
Rais Magufuli  na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea Nzega Mkoani Tabora.
7
Rais Magufuli akiwa na wabunge wa Mkoa wa Singida wakati akiwahutubia wakazi wa Misigiri Mkoani Singida wakati akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora.
8.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na wabunge wa Singida
5
Rais Magufuli katika Kijiji cha Nanga Wilayani Igunga mkoani Tabora.
1. 1146

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad