MATOKEO / RATIBA VPL 2015/2016:-Azam FC walishindwa kulinda Uongozi wa bao 2-0 na kutoka Sare na JKT Ruvu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 05, 2016

MATOKEO / RATIBA VPL 2015/2016:-Azam FC walishindwa kulinda Uongozi wa bao 2-0 na kutoka Sare na JKT Ruvu.

Wana lambalamba Azam FC walishindwa kulinda uongozi wa bao 2-0 na kutoka Sare 2-2 na JKT Ruvu katika Mechi ya  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyochezwa huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam .
Bao za Azam FC zilipatikana dakika za 31 na 37  kupitia kwa  Bolou na Kipre Tchetche na JKT Ruvu kusawazisha Kipindi cha Pili Dakika za 56, kwa Penati ya Saadi Kipanga, na Bao jingine ni la Dakika ya 71 la Najim Magulu.

Huku kila Timu ikiwa imebakiza Mechi 3, Yanga SC wanaongoza Ligi kuu wakiwa na Pointi 68 wakifuata Azam FC wenye Pointi 60 na Simba SC ya 3 ikiwa na Pointi 58 wakiwa na Mechi 4 mkononi.

Hali hii inaifanya Yanga SC kuhitaji Pointi 3 tu katika Mechi zao 3 zilizobaki ili watwae tena Ubingwa bila kujali matokeo ya Azam FC na Simba SC.

Lakini pia upo uwezekano wa Yanga SC kutwaa bila ya hata kutwaa hizo Pointi 3 kwa vile Azam FC na Simba SC zina Mechi zao Mei 8 na Yanga SC Mechi yao inayofuata ni Mei 10 na ikiwa Azam FC na Simba SC zitateleza kwenye Mechi zao za Siku hiyo basi Yanga SC atangazwa Bingwa Siku hiyo hiyo.

LIGI KUU VODACOM 2015/2016 - RATIBA                                              

Jumamosi Mei 7,2016.

JKT Ruvu v Ndanda FC

Stand United v Coastal Union

Mgambo JKT v Mtibwa Sugar

Jumapili Mei 8,2016.

Tanzania Prisons v Majimaji

Simba v Mwadui FC

Kagera Sugar v Azam FC

Jumanne Mei 10,2016.

Mbeya City v Yanga SC

Jumatano Me 11,2016.

Majimaji v Simba SC

Jumamosi Mei 14,2016.

Mgambo JKT v JKT Ruvu

Ndanda FC v Yanga SC

Jumapili Mei 15,2016.

Mtibwa Sugar v Simba SC

Kagera Sugar v Stand United

Mwadui FC v Mbeya City

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad