FAINALI KLABU BINGWA ULAYA 2015/2016:-Ni May 28,2016 Real Madrid na Atletico Madrid. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 05, 2016

FAINALI KLABU BINGWA ULAYA 2015/2016:-Ni May 28,2016 Real Madrid na Atletico Madrid.

Manchester City ya uingereza wameshindwa kufika katika fainali ya kwanza ya Klabu Bingwa barani Ulaya ( UEFA 2015/2016 ) baada ya kutolewa na Mabingwa mara 10 wa michuano hiyo Real Madrid ya Hispania katika mchezo uliokua wa kuvutia tena wa aina yake.

Nyota wa Real Madrid, Gareth Bale akipiga shuti linalombabatiza beki wa Manchester City, Fernando na kuipatia timu yake bao pekee la ushindi Uwanja wa Bernabeu katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Real Madrid inatinga fainali kwa ushindi wa jumla wa 1-0 baada ya awali kutoa sare ya 0-0 mjini Manchester.


Real Madrid sasa watakutana na Atletico Madrid katika uwanja wa San Siro tarehe 28, Mei,2016, hii ikiwa ni kama marudio ya fainali za mwaka 2014 ambapo Real Madrid walishinda kwa mabao 4-1 baada ya muda wa nyongeza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad