TANGAZO LA KAZI:-Changamkia Nafasi 26 za Kazi wilayani Ngara/kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 05, 2016

TANGAZO LA KAZI:-Changamkia Nafasi 26 za Kazi wilayani Ngara/kagera.


MOORLAND PREMIER HOTELS LIMITED

CCM/MURGWANZA ROAD – NGARA
S. L. P 223
NGARA – KAGERA
NORTH WESTERN OF TANZANIA
Simu: +255 787 370 633/786 803 878/754 979 868/758 421 849
01/05/2016

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI (26)

Moorland Premier Hotels and Tours Limited ni Hotel Mpya na ya Kisasa inayotaraji wa Kufunguliwa rasmi ndani ya mwaka huu wa 2016 Msimuwa Mavuno (Fiesta time). 

Iko katika hatua za mwisho kukamilika na inatarajiwa kutoa ajira za kudumu na za muda kwa wazalendo na wageni wasiopungua arobaini (40) ndani ya Wilaya ya Ngara na njeya Wilaya. 

Hotel ipo Wilayani Ngara Karibu na Kituo Cha Police/Magereza 0.5km Kutoka Barabara kuu (High way) ya kwenda Kabanga/Burundi Boarder, Ofisi ya CCM, Barabara ya Murgwanza Hospital, Mkoani Kagera, Kasikazini Magharibi nchini Tanzania.

Uongozi wa Hotel unapenda Kuwatangazia Nafasi za Kazi Kama ifuatavyo:

1. Hotel Manager/Meneja wa Hotel - Nafasi (1)

2. Mapokezi/Receiptionist (2)

3. Wapishi/Cooks - Nafasi (4)

4. Wahudumu/Bar & Kitchen Attendants – Nafasi (8)

           5. DJ – (Disco Joker/Mchezesha Mziki) – Nafasi moja (1)

           6. Walinzi/Security Guards – Nafasi Mbili (2)

           7. Mtunza Stoo/Store kepeer- Nafasi Moja (1)

           8. Wafanya Usafiwa Ndani/House Keepers/Washers – Nafasi tano (5)

           9. Mfanya usafiwa Mazingira/Garderner – Nafasi Moja (1)

            10. Mhudumu/Attendant M-Pesa (Vodacom, Airtel Money, Tigo Pesa, NMB, CRDB Bank na RIFARO/Selcom) Wakala – Nafasi Moja (1)

Waombaji/Muombaji wawe/awe na sifa zifuatazo Kiujumla:-

·      Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka kumi na nane (18yrs) na Kuendelea

·      Awe na Hati ya Kuzaliwa ya Tanzania au Kitambulisho cha Makazi yake

·      Awe anajua kusoma na Kuandika Kiswahili, Kiingereza au Kifaransa

·      Awe na Elimuya Kuanzia Kidato Cha nne na Kuendelea

·      Awe hajawahi Kuhusika na kesi ya aina yoyote ya Police ama Kufikishwa Mahakamani

·      Awe Tiyari Kufundishwa na Kufundisha pale inapobidi

·      Awe Mbunifu na Mwenye Kujituma bila kushurutishwa

·      Awe Mkarimu/Hospitality kwa wageni na Mwaminifu kwa Mwajiri wake

·      Awe na uzoefu wa kazi kwa nafasi husika kuanzia Miaka miwili (2) na Kuendelea

·      Awe na Vyeti vya Uzoefu Kwenye Kazi husika, Vyenye anuani na namba za simu au barua pepe za mwajiri wake sehemu alipofanya kazi au anapofanya kazi kwa sasa

·      Awe tiyari Kuwajibika au kuwajibishwa pale inapobidi

Ngongeza ya sifa Kwa Nafasi baadhi hapo Juu:

1.     Hotel Manager/Meneja wa Hotel/ Mapokezi/Receiptionists/Wahudumu/Bar & Kitchen Attendants

·      Awe Amehitimu masomo ya utawala wa Hotel na Utalii/Hotel Management and Tour  Guides na awe na cheti cha chuo kinachotambulika

·      Awe amehudhulia Semina mbalimbali za uongozi Shupavu na awe na vidhibitisho.

·      Aliyesoma masomo ya Komputa na Anaye jua Kutumia komputa atapewa kipa umbele zaidi

2.     Wapishi/Cooks

·      Awe Amehitimu masomo ya utawala wa Hotel na Utalii/Hotel Management and Tour Guides na awe na cheti cha chuo kinachotambulika.

·      Awe amehudhulia Semina mbalimbali za Upishi na awe navidhibitisho

·      Awe anajua Kutengeneza Menu ya Siku, ya wiki na ya Mwezi

·      Awe anajua kusoma na kuitafsiri Menu kwa wateja/Wageni

3.     Kwa walinzi/Security Guards

·      Atakaye kuwa na cheti cha kuhitimu mafunzo ya Mgambo au kozi yoyote ya ulinzi kwenye shule ama chuo kinachotambulika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapewa Kipaumbele

4.     Mtunza Bustani/Garderner: 

·      Anayejua Kutumia vizuri na Kutengeneza Mashineya Kukata Nyasi yenye injini ya Petrol atapewa kipaumbele

5.     DJ – Disco Joker/Mchezesha Mziki: 

·      Mwenye Vyeti Vya Chuo Cha sanaa na Utamaduni kilichosajiliwa na BASATA (Baraza la Sanaa Tanzania) na Kutambuliwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenye uzoefu kazini pia akiwa na Tanzania Driving Licence atapewa Kipaumbele

6.     Mhudumuwa M-Pesa/M-Pesa Attendant:

·      Aliyesoma masomo ya Komputa na Anaye jua Kutumia komputa atapewa kipa umbele zaidi

Mwenye sifa zote hapo juu ataitwa kufika kwenye Mchujo/Interview kupitia namba zake za simu au Barua Pepe atakazo kuwa ametuandikia kwenye barua yake ya maombi.

Gharama za Usafiri wa kuja na kurudi ulikotoka wakati wa mchujo/Interview Pamoja na za Chakula na Kulala ni za kwako mwenyewe

Mwisho wa Kupokea Maombi ni Tarehe 25/5/2016 Saa nne (4:00) Asubuhi

Maombi yatumwe Kwenye Anuani Tajwa hapo juu, au kwenye baruapepe ya mphngara@gmail.com au yafikishwe Paradise Hotel/Restaurant – Nakatunga Ngara (TZ) na ya ambatanishwe na kopi za vyeti vyako vya origino.

Ukituma maombi na ikafika tarehe 31/05/2016 Kabla haujaitwa au kupigiwa simu kwa namba yoyote kati ya hizo hapo juu kwenye anuani yetu, Tafadhali usitupigie simu, tambua kuwa Barua yako na vyeti vyako hatujaridhika navyo.

Moorland Premier Hotel itakua na masilahi mazuri na malengo mazuri ya kukuza na kuendeleza vipaji vya wafanya kazi kwa kupitia mafunzo mbalimbali kwa kazi husika.

 – Mishahara ni makubaliono baada ya Mchujo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad