UP DATE /AJALI /PICHA:-Mtu mmoja afariki katika ajali ya gari na 4 wamejeruhiwa akiwemo mama Tunu Pinda Mkoani Morogoro. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 08, 2016

UP DATE /AJALI /PICHA:-Mtu mmoja afariki katika ajali ya gari na 4 wamejeruhiwa akiwemo mama Tunu Pinda Mkoani Morogoro.

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa akiwemo mke wa waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda baada ya gari walilokuwa wakisafiria kumgonga mwendesha pikipiki wakati akikatisha barabara katika eneo la Mkundi barabara ya Morogoro Dodoma manispaa ya Morogoro.

Ajali hiyo imetokea leo February 08,2016, majira ya saa nane mchana katika eneo la Mkundi ikihusisha gari lenye namba za usajili STK 9242 gari la mke wa waziri mstaafu Mizengo Pinda likitokea Dodoma kwenda jijini Dar-es-Salaam  na pikipiki.
Majeruhi wengine wa ajali hiyo ni dereva wa gari hilo Bw Anjelo Mwisa, mlinzi wa mke wa waziri mkuu mstaafu Gaudensi Tembo na kijana wa familia ya Mama Tunu Pinda Bwana Gilbert Sampa.

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Dr Rita Liamuya amesema hali ya mke wa waziri mkuu mstaafu na majeruhi wengine zinaendelea vizuri na kueleza kuwa  majeruhi hao wanatarajia kuhamishiwa jijini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi.
Muonekano wa gari lenye namba za usajili STK 9242 gari la mke wa waziri mstaafu Mizengo Pinda likiwalimeharibika vibaya baada ya kupata ajali leo February 08,2016.

Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630 Or+255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad