SHERIA ZETU:-Yona na Mramba Waanza Kifungo cha Nje. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 08, 2016

SHERIA ZETU:-Yona na Mramba Waanza Kifungo cha Nje.

12.Yona akishuka katika gari lililowaleta hospitalini hapo.
Daniel Yona akishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili Hospitali ya Palestina, Sinza – Dar es Salaam leo Jumatatu,February 08,2016.

1.Wakikabidhiwa vifaa vya kufanyia usafi katika hospitali ya Palestina.
Yona na Mramba  wakiwa wameshika vifaa vya kufanyia usafi.

2.Yona akiwa ameshika fagio na fyekeo atakalofanyia usafi katika Hospitali ya Parestina.
3.
4.Hali ilivyoonekana katika Hospitali hiyo.
Wakioneshwa mazingira ambayo watakuwa wakiyafanyia usafi kwa kipindi chote cha adhabu.

6.Yona akikabidhiwa mavazi maalum ya kufanyia shughuli ya usafi kutoka kwa afisa mazingira wa hospitali ya Parestina,Miriam Mongi (katikati).
Ofisa Mazingira wa Hospitali ya Palestina-Sinza, Bi. Miriam Mongi (mwenye brauzi nyekundu) akimkabidhi Yona vifaa vya kufanyia usafi.

7.Yona na Mramba wakiwa wamevaa mavazi maalum kwa ajili ya kufanyia usafi.
Yona na Mramba wakiwa wamevaa ‘ovaroli’.


DSC_0088
Ofisa Huduma za Jamii wa Hospitali ya Palestina – Sinza, Bw. Deogratius Shirima akizungumza na wanahabari hospitalini hapo.

8.Baadhi ya eneo watakalolisafisha ndani ya hospitali hiyo.
Maeneo ya hospitalini hapo.

9.Gari walilokuja nalo hospital;ini hapo..
10.Mmoja wa raia aliyeguswa na adhabu hiyo ya akionesha hisia zake kuwakaribisha walipofika hospitalini hapo.11
Takataka  katika baadhi ya maeneo hospitalini hapo.

DSC_0001
DSC_0002
Wanahabari wakichukua matukio.
DSC_0005
Waliokuwa Mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona ,leo Jumatatu,February 08,2016 wameanza kutumikia adhabu ya kifungo cha nje, kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza, Palestina, ya jijini Dar, kulingana na hukumu iliyotolewa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wiki iliyopita kuhusu kesi iliyokuwa ikiwakabili.

Mramba aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini waliwasili mapema leo majira ya saa 3:30 asubuhi katika Hospitali ya Sinza Palestina ili kuanza kutumikia adhabu hiyo kama mahakama ilivyowaamuru.

Baada ya kuwasili hospitalini hapo, Yona na Mramba walipokelewa na ofisa huduma za jamii Bw. Deogratius Shirima na Wananchi wengine waliokuwepo kushuhudia vigogo hao wakitumikia adhabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, Shirima alisema kuwa, leo ilikuwa ni siku ya kuwapa maelekezo namna ambavyo watafanya usafi, maeneo ya kufanya usafi pia walikabidhiwa vifaa watakavyovitumia kufanyia usafi kuanzia kesho.

Baadaye Afisa Mazingira hospitalini hapo Bi. Miriam Mongi, aliwakabidhi Yona na Mramba vifaa vya kufanyia usafi ambavyo ni; mifagio, mafyekeo, viatu vya kufanyia usafi maarufu kama “gambuti” na glovusi.

Oktoba 2, 2015 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona ambapo Jaji Projest Rugazia, alikubaliana na hoja kwamba kwa mujibu wa mashtaka yaliyowatia hatiani kwa matumizi mabaya ya Ofisi na kwa mujibu wa kifungo cha 35 cha adhabu PC ambacho mahakama ilikitumia walipaswa kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili na si miaka mitatu.

Mawaziri hao wa zamani waliwasilisha barua hiyo ya kuitaarifu mahakama yenye kumbukumbu namba 151/DA/3/11/223 ya Desemba 5, mwaka jana, wakiongozwa na jopo la mawakili wao watatu Peter Swai, Cuthbert Nyange na Elisa Msuya ndipo hivi karibuni baada ya mahakama kupitia upya kesi hiyo ikaamuru wapewe adhabu ya kifungo cha nje huku wakifanya kazi za kijamii kwa muda wa saa nne kila siku kwa miezi sita.
 
Na Denis Mtima/GPL.


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630 Or+255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad