KAMATI KUU CCM:-Wafahamu Wagombea walioteuliwa kujaza Nafasi mbali mbali zilizo wazi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 08, 2016

KAMATI KUU CCM:-Wafahamu Wagombea walioteuliwa kujaza Nafasi mbali mbali zilizo wazi.

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
 
Jana tarehe 07/02/2016 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilikuwa na kikao maalum cha siku moja mjini Dodoma. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. 

Kikao hicho kilikuwa na kazi ya kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali zilizo wazi za uongozi ndani ya CCM mikoani na wilayani ambazo uteuzi wake upo kwenye Mamlaka ya Vikao vya Chama Taifa.
Nafasi hizi wazi zimetokana na sababu mbalimbali zikiwemo vifo na baadhi ya viongozi kukihama Chama na kujiunga na vyama vingine. Hivyo, nafasi zilizofanyiwa uteuzi na wagombea wake ni kama ifuatavyo:-

I.     UENYEKITI WA CCM MKOA.

1.      ARUSHA
(i)      Michael Lekule Laizer
(ii)     Emanuel Makongoro Lusenga
(iii)   John Pallangyo

2.   SHINYANGA
(i)      Hassan Ramadhani Mwendapole
(ii)     Mbala Kashinje Mlolwa
(iii)   Erasto Izengo Kwilasa

3.   SINGIDA
(i)    Hanje Narumba Barnabas
(ii)   Misanga Mohamed Hamis
(iii)  Mlata Martha Moses
(iv)  Kilimba Juma Hassan

II.     UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NEC

1.       NYAMAGANA
(i)    DR. Sillinus Elias Nyanda
(ii)   Jamal abdul Babu
(iii)  Kelebe Bandoma Lutelil
(iv)  Patrick Kambarage Nyabugongwe

2.       KAHAMA
(i)   Pili Yakanuka Izengo
(ii)  Paschal Ndibatyo Mayengo
(iii) Sweetbert Charles Nkuba
3.       MONDULI
(i)  Namelock Edward Sokoine

III.    UENYEKITI WA CCM WILAYA

1.       MONDULI
(i)  Loata Erasto Sanare

2.       SUMBAWANGA MJINI
(i)  Chami Slegried Mask
(ii) Godfrey Mwimanzi Mwikala

IV. KATIBU WA UCHUMI NA FEDHA MKOA WA KILIMANJARO

(i)    Shadrack Amani
(ii)   Chata Madata Joseph
(iii)  Karia Ahmed Mahamoud

V.      KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA ARUSHA
(i)   Semmy Rabson Kiondo
(ii)  Shaban Omari Mdoe
(iii) Veraikunda Zablon Urio

VI.     UENYEKITI WA UVCCM WA MKOA

1.   ARUSHA
(i)            Erick Edward
(ii)            Lengai Loy Thomas
(iii)          Mwanzani Omar

  2.   KILIMANJARO
(i)      Amaly T.Mathew
(ii)     Frank Lumisha Nkya
(iii)   Juma Rahibu Juma

2.   SHINYANGA
                (i)   Mabembela Joseph Elias
                (ii)  Mipanda kali Dalushi
                (iii) Ndasa Jeremiah Damian
                (iv) Shigela Reubeen Bernard

Ratiba ya chaguzi hizo itatolewa wiki hii mwishoni.

Kamati Kuu pia imepokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi wa marudio Zanzibar na kuridhishwa na maandalizi hayo na kuwatakia kila la kheri Wazanzibar katika Uchaguzi huo.

Wakati huo huo, Kamati Kuu imetoa pole kwa Jeshi la Polisi nchini kufuatia vifo vya Askari Polisi watatu vilivyotokea tarehe 06/02/2016 mjini Singida kutokana na ajali wakati Askari hao wakitimiza wajibu wao kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM. Kamati Kuu inawapa pole wafiwa wote na kuwaombea majeruhi wote kupona haraka.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
08/02/2016.
 
Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630 Or+255756830214.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad