MAFANIKIO:-Rais Magufuli Ampongeza Mbwana Ally Samatta Kwa Kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 08, 2016

MAFANIKIO:-Rais Magufuli Ampongeza Mbwana Ally Samatta Kwa Kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika 2015.

Jana,January 7, 2016 Tanzania iliandika historia  katika medali ya soka Afrika na duniani baada ya mshambuliaji Mtanzania anakipiga katika klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta kushinda tuzo ya Mwanasoka bora wa Afrika,2015 kwa wachezaji wanaocheza Afrika.

Mbwana Samatta alitangazwa mshindi huko Abuja, Nigeria katika tuzo zilizowashirikisha mastaa mbalimbali wa soka Afrika.

 Furaha ya Watanzania pia imemgusa Rais wa awamu ya tano Dkt John Magufuli ambaye ametuma pongezi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye.

Katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, Rais amemtaka Waziri Nape amfikishie salamu za pongezi mchezaji huyo na pia tuzo hiyo imemjengea heshima kubwa na kuleta heshima kwa wachezaji wa Tanzania.

Taarifa hiyo ilisomeka hivi..

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad