TASWIRA PICHA:- Mbwana Aly SAMATTA na Pierre-Emerick AUBAMEYANG wakiwa na Tuzo ya Ubora Barani Afrika. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 08, 2016

TASWIRA PICHA:- Mbwana Aly SAMATTA na Pierre-Emerick AUBAMEYANG wakiwa na Tuzo ya Ubora Barani Afrika.

Aubameyanga amefana sana akichezea Borussia Dortmund.

BUNDESLIGA TOP SCORERS 2015/2016.

Aubameyang (Dortmund) – 18

Lewandowski (Bayern Munich) – 15

Muller (Bayern Munich) – 14

Hernandez (Bayer Leverkusen) – 11

Kalou (Hertha Berlin) – 9.
Mbwana Samatta akipokea tuzo yake ukumbi wa mikutano wa kimataifa mjini Abuja,Nigeria.

Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika.

Mbwana Samatta amepata pointi 127, mbele ya mchezaji mwenzake wa TP Mazembe, kipa Robert Muteba Kidiaba wa DRC, aliyepata pointi 88, wakati mshambuliaji wa Etoile du Sahel ya Tunisia na timu ya taifa ya Algeria, Baghdad Bounedjah amepata pointi 63.

Mafanikio ya Samatta anayeweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo kubwa ya Afrika, yanakuja baada ya kuiwezesha TP Mazembe kutwaa taji la tano la Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake nane.
Pierre-Emerick Aubameyang (kushoto) akipokea tuzo yake kutoka kwa Rais wa CAF, Issa Hayatou.

Tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika imemwendea Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kambumbu katika klabu ya Borussia Dotmund nchini Ujerumani,ikiwa ni Tuzo yake kwa mara ya kwanza.

Mchezaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani mwenye umri wa miaka 26, amewaangusha Yaya Toure wa Ivory Coast aliyekuwa anashikilia tuzo hiyo na Andre Ayew wa Ghana.

Amekusanya pointi 143, saba zaidi ya Toure wakati Ayew ameshika nafasi ya tatu kwa kupata pointi 112 na anakuwa mchezaji wa kwanza wa Gabon kushinda tuzo ya CAF
Kiungo wa Nigeria, Etebo Peter Oghenekaro ameshinda tuzo ya Mchezaji Anayechipukia Vizuri dhidi ya Mnigeria mwenzake, Azubuike Okechukwu, kipa wa Mali, Djigui Diarra, Mahmoud Abdelmonem Abdelhamid ‘Kahraba’ wa Misri na Mualgeria, Zinedine Ferhat.
Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF ,zimetolewa usiku wa kuamkia Ijumaa January 8, 2016,mjini Abuja nchini Nigeria.

Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Ivory Coast.

Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon.

Kocha bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Ivory Coast, tuzo ambayo ameishinda kwa mwaka wa pili mfululizo.

Klabu bora ya soka barani Afrika ni TP Mazembe, kutoka DR Congo.

Mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon.

Mwamuzi bora wa mwaka ni Bakary Gassama kutoka nchini Gambia.

Tuzo hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria Omowumi.

KIKOSI BORA AFRIKA

Kipa: Robert Muteba KIDIABA (DRC)

Mabeki: Serge AURIER (Ivory Coast), Aymen ABDENNOUR (Tunisia), Mohamed MEFTAH (Algeria)

Viungo: Andre AYEW (Ghana), Yaya TOURE (Ivory Coast), Sadio MANE (Senegal), Yacine BRAHIMI (Algeria),  
  
Washambuliaji: Mbwana Aly SAMATTA (Tanzania), Pierre-Emerrick AUBAMEYANG (Gabon), Baghdad BOUNEDJAH (Algeria)

WACHEZAJI WA AKIBA

Djigui DIARRA (Mali)

Azubuike OKECHUKWU (Nigeria)

Kelechi NWAKALI (Nigeria)

Zinedine FERHAT (Algeria)

Adama TRAORE (Mali)

Victor OSIMHEN (Nigeria)

Kermit ERASMUS (Afrika Kusini)

LAST 10 WINNERS

2005: Samuel Eto'o, Barcelona

2006: Didier Drogba, Chelsea

2007: Frederic Kanoute, Sevilla

2008: Emmanuel Adebayor, Arsenal

2009: Didier Drogba, Chelsea

2010: Samuel Eto'o, Inter Milan

2011: Yaya Toure, Manchester City

2012: Yaya Toure, Manchester City

2013: Yaya Toure, Manchester City

2014: Yaya Toure, Manchester City

2015: Pierre-Emerick Aubameyang, Borussia Dortmund


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad