BARAZA LA MAWAZIRI TANZANIA 2015-2020:-Sasa lina Mawaziri 19 tu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 10, 2015

BARAZA LA MAWAZIRI TANZANIA 2015-2020:-Sasa lina Mawaziri 19 tu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na wanahabari waliofika kumsikiliza wakati akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa walioketi vitini ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue..BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BARAZA LA MAWAZIRI

Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.

Mawaziri - George Simbachakene  na Angella Kairuki.

Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira.

Waziri - January Makamba

Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu.

Waziri - Jenista Muhagama

Ma-Naibu Waziri – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Waziri - Mwigulu Nchemba

Naibu Waziri - William Ole Nasha

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Waziri - Bado hajapatikana.

Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani

Wizara ya Fedha na Mipango.

Waziri - Bado hajapatikana.

Naibu Waziri - Ashantu Kizachi

Wizara ya Nishati na Madini.

Waziri - Prof. Mwigalumi Muhongo.

Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.

Wizara ya Katiba na Sheria.

Waziri - Harrison Mwakyembe

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Waziri - Dk. Augustino Mahiga

Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Waziri - Dk. Hussein Mwinyi

Wizara ya Mambo ya Ndani.

Waziri - Charles Kitwanga.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waziri - William Lukuvi

Naibu Waziri - Angelina Mabula

Wizara ya Maliasili na Utalii.

Waziri - Bado hajapatikana.

Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Waziri - Charles Mwijage.

Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.

Waziri - Bado hajapatikana.

Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Waziri - Ummy Mwalim

Naibu Waziri  Dkt. Hamis Kigwangala

Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo.

Waziri - Nape Nnauye

Naibu Waziri - Anastasia Wambura.

Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Waziri – Prof. Makame Mbarawa

Naibu  Waziri– Inj. Isack Kamwela

Rais Magufuli amefafanua wakati wa Kutangaza baraza hilo kuwa'' - Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza.

Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri.

Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad