TAZAMA PICHA :-Za uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege kiwanja cha Pemba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 08, 2016

TAZAMA PICHA :-Za uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege kiwanja cha Pemba.

Aina ya Taa zilizokuwa mwishoni mwa kiwanja cha ndege cha Karume Pemba zikiwa na Rangi ya Nyekundu na Buluu ambazo hutoa ishara kwa Kepteni anayeongoza Ndege ikitua,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongozi mbali mbali aliofuatana nao walijionea  taa hizo namna zilivyofungwa  katika utaratibu maalum wakati  uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba uliofanyika jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Aina ya Taa zilizokuwa nje kabisa ya  kiwanja cha ndege cha Karume Pemba  ambazo hutoa ishara kwa Kepteni anayeongoza Ndege ikitua,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongozi mbali mbali aliofuatana nao walijionea  taa hizo namna zilivyofungwa  katika utaratibu maalum wakati  uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba uliofanyika jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifungua pazia kama iskara ya Uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege katika kiwanja cha Ndege cha Karume Pemba jana ikiwa ni katika sherehe za shamra shamra za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi(GAVU).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ngege Zanzibar Kepten  Saidi Iddi Ndumbugani, kuhusu majenereta yanayotoa umeme baada ya kuzindua rasmi  Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

 [Picha na Ikulu.]

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad