![]() |
|
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akionesha kwa
msisitizo Picha rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati wa mkutano na Vyombo vya habari leo
Jijini Dar es salaam.
PICHA Rasmi
ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuri
imetoka leo Januari 8, 2015 katika Ofisi ya Idara ya Habari (MAELEZO) Dar es Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Kaimu Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zamaradi Kawawa, amesema kuwa Picha hiyo ya
Rais Magufuri kwa kila moja itauzwa kwa
sh15000 ya kitanzania bila ya kuwekwa frem,huku picha ya Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere itauzwa kwa sh 5000.
Aidha
Zamaradi amesema kuwa Nakala za picha hizo zinapatikana Idara ya Habari
Maelezo na Ofisi za Wakala wa Huduma ya
Ununuzi Serikalini (GPSA).
Picha hiyo
ya Rais pamoja na ya Baba wa Taifa zinatakiwa
kutundikwa katika ofisi zote za Serikali,Taasisi za Umma,Mashirika na Ofisi
Binafsi.
Aidha
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Raphael Hokororo amesema picha
ya Rais Magufuri imewahi kutoka mapema sana kuliko picha za Waheshimiwa
waliopita na kusema kuwa hairuhusiwi
kukopi wala kunakili picha hiyo.
Serikali
inatoa onyo kwa wale wote wanaosambaza picha isiyo rasmi pamoja na Serikali
kusitisha matumizi ya picha hiyo na wale wote wanaotengeneza picha ukubwa usio
rasmi, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.Kwani Idara ya Habari Maelezo
ndiyo yenye Haki miliki ya picha hiyo.
|
Friday, January 08, 2016
Home
HABARI
TAARIFA KWA UMMA:-Serikali ya Tanzania yatoa Picha Rasmi ya Rais ,Dkt John Pombe Magufuli.
TAARIFA KWA UMMA:-Serikali ya Tanzania yatoa Picha Rasmi ya Rais ,Dkt John Pombe Magufuli.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment