VPL – 2015/2016:-Azam FC v Simba SC na Mgambo JKT v Yanga SC kesho December 12,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 11, 2015

VPL – 2015/2016:-Azam FC v Simba SC na Mgambo JKT v Yanga SC kesho December 12,2015.

Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara , VPL – 2015/2016, kesho Jumamosi December 12 na 13,2015 inarejea kwa kishindo kwa mitanange mikali ikiwepo ile Mechi ya mvuto mkubwa kati ya Vinara wa Ligi Azam FC na Simba SC huku Mabingwa Watetezi Yanga SC wakiwa Mkwakwani, Tanga kucheza na Mgambo JKT wakati Jumapili Uwanjani hapo hapo ipo Dabi ya Tanga kati ya Coastal Union na African Sports.

Baada ya Mechi 9 Azam FC wapo juu kwenye VPL wakiwa na Pointi 25 wakifuatiwa na Mabingwa Watetezi Yanga SC wenye Pointi 23 kisha Mtibwa Sugar Pointi 22 na Simba SC wapo Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 21.

Kwenye Mechi za Wikiendi hii, huenda baadhi ya Timu zikawa zina Wachezaji wapya baada ya kuimarisha Vikosi vyao kwa kutumia Dirisho la Uhamisho la Kipindi hiki.

Simba SC wao wamemrejesha Straika kutoka Kenya, Paul Kiongera, na pia kuwanunua Beki wa African Sports, Novat Makunga, na Straika wa Mtibwa Sugar Haji Ugando.

Azam FC wao wamemchukua Kipa Ivo Mapunda ambae alizidakia Klabu kubwa hapa Nchini nan je ya Nchi alipokuwa na Gor Mahia ya Kenya na Saint George ya Ethiopia.

LIGI KUU VODACOM 2015/2016 -RATIBA

Jumamosi Desemba 12,2015.

Kagera Sugar v Ndanda FC

Stand United v Mwadui FC

Mbeya City v Mtibwa Sugar

Azam FC v Simba SC

Majimaji v Toto Africans

Mgambo JKT v Yanga SC

Jumapili Desemba 13,2015.

JKT Ruvu v Tanzania Prisons

Coastal Union v African Sports

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

Post Bottom Ad