VPL 2015/2016:-Tazama Matokeo yote ya Ligi Kuu Bara leo hii December 12,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 12, 2015

VPL 2015/2016:-Tazama Matokeo yote ya Ligi Kuu Bara leo hii December 12,2015.

Dar es Salaam derby kati ya Azam FC ambao walikuwa wenyeji wa mchezo wa leo December 12,2015 dhidi ya ‘mnyama mnyamani’ Simba SC  imemalizika kwa sare ya kufungana magoli 2 - 2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Matokeo hayo, yanaifanya kila timu ijiongezee pointi moja, Azam FC ikifikisha 26 na Simba SC ikitimiza 22 baada ya timu zote kucheza mechi 10. 

Azam FC inaendelea kuwa kileleni baada ya Yanga SC nayo kulazimishwa sare ya 0-0 na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga jioni ya leo hivyo kufikisha pointi 24, wakati Simba SC ikibaki nafasi ya nne.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

Post Bottom Ad