![]() |
Na Gibson
Mika -RK Geita 90.5 FM.
Kushoto
Anayesaini ni Mkurugenzi Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu na Buzwagi Bw.Benedict
Busunzu , Kulia kwake Ni Mkurugenzi wa
Wilaya ya Nyang'hwale Bi Mariam Chaulembo.
|
![]() |
Picha ya
Pamoja ya Viongozi wa Mgodi, Viongozi wa Mkoa Ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Geita, Mhandisi Robart Gabriel
Pamoja na Viongozi wa Wilaya Nyang’hwale.
Kufuatia
upungufu wa vituo vya afya na zahanati katika wilaya ya Nyang’hwale Mkoani
Geita, Mgodi wa Bulyanhulu kupitia kampuni ya ACACIA uliopo mkoani
Shinyang’a wameingia makubaliano na halmashauri ya wilaya hiyo katika
ukamilisha wa majengo ya zahanati 32 ili kuwasaidia wananchi kupata huduma za
matibabu .
Akizungumza
baada ya kutiliana saini na Uongozi wa Mgodi huo Mkuu wa mkoa wa Geita,
Mhandisi Robart Gabriel amesema
wamekubaliana na uongozi wa mgodi kutoa kiasi cha shilingi milioni 500 kwa
ajiri ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati katika vijiji 32 ili kuwasaidia
wananchi kuepukana na changamoto ya kutembea umbali mrefu wakitafuta huduma za
matibabu.
|
![]() |
Balaza la
Madiwani Nyang'hwale.
Nae Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu na Buzwagi Bw, Benedict Busunzu amesema hatua hiyo itapunguza changamoto ya
wananchi kutembea umbari mrefu wakitafuta huduma za matibabu na kuleta mapinduzi
ya kimaendeleo hasa katika sekta ya afya.
Aidha
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi Mariam
Chaulembo ameushukuru mgodi huo na kuhahidi kusimamia fedha hizo ili ziweze
kakamililisha ujenzi wa maboma hayo kwa wakati na wananchi kuanza kunufaika na miradi
hiyo.
|
No comments:
Post a Comment