ZOGO BUNGENI JULAI 03,2015:-Hii ndio Marufuku iliyotolewa kwa Hawa Wabunge kuingia bungeni. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 04, 2015

ZOGO BUNGENI JULAI 03,2015:-Hii ndio Marufuku iliyotolewa kwa Hawa Wabunge kuingia bungeni.

Jana Julai 03,2015 imekuwa siku nyingine ambayo kikao cha Bunge la Tanzania huko mkoani  Dodoma kutoisha kwa amani, Wabunge wa Upinzani kwa mara nyingine walipinga Bunge kuendelea kujadili miswada ambayo iliwasilishwa.

Baada ya Kikao cha Bunge kuahirishwa asubuhi, Jioni Kikao kiliendelea tena ambapo kwanza ilisomwa taarifa kuhusu ishu ya utata uliotokea Bungeni kuwasilishwa kwenye Kamati ya Maadili na yakatolewa maamuzi ya Kamati hiyo.” hayo maneno ameyasema Mwenyekiti wa Kamati, Hassan Ngwilizi.



“Vitendo vilivyofanywa na Wabunge hao ni ukiukaji wa Kanuni za Bunge… Kamati imeamua Wabunge Tundu Lissu, John Mnyika, Moses Machali, Pauline Gekuu na Felix Mkosamali wasihudhurie vikao vyote vilivyosalia kwenye mkutano wa 20 kuanzia tarehe 4 Julai 2015” – Hassan Ngwilizi.

“Kamati pia imeamua wabunge Rajabu Mbarouk na Mchungaji Peter Msigwa wasihudhurie vikao viwili vya mkutano wa Bunge kuanzia tarehe 4 Julai 2015, na Wabunge Joseph Selasini, Khalifa Suleiman Khalifa na Rashid Ali Abdallah wanatakiwa kufika mbele ya kamati ya maadili Jumamosi saa nne asubuhi kwa kuwa hawakupata hati ya kuitwa kwa haraka.” >>> Mwenyekiti wa kamati ya haki, kinga na maadili ya Bunge, Brigedia Mstaafu Hassan Ngwilizi.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad