UHALIFU:-Abiria wa Basi alazimika kutimua mbio baada ya Sanduku lake kukutwa na Bangi zaidi ya Kilo 25. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 04, 2015

UHALIFU:-Abiria wa Basi alazimika kutimua mbio baada ya Sanduku lake kukutwa na Bangi zaidi ya Kilo 25.

Abiria wa basi la Maning’Naice lililokuwa likitoka Mtwara kwenda Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina la Shaibu Rajabu amelazimika kutimua mbio na kuishia porini baada ya sanduku alilokuwa amebeba kubainika limeshindiliwa dawa za kulevya aina ya bangi inayosadikiwa kuwa na zaidi ya kilo 25.

Tukio hilo limejitokeza eneo la Nangurukuru baada ya polisi kusimamisha basi hilo na kufanya upekuzi wa mizigo na ndipo walipokutana na dhahama hiyo .

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renatha Mzinga amethibitisha kwa njia ya simu kukamatwa kwa bangi hiyo ambayo amesema ni kilo tano huku akikiri mara nyingi wanaikamata na wasafirishaji wanatokea mkoani Mtwara.



Kuna mtu mmoja aliteremka akasema ana mkojo.. Askari akauliza nani mwenye hili begi yule jamaa akaanza kukimbia vichakani. Askari wakakimbizana nae maporini, akatokomea“– amesimulia dereva wa basi hilo, Hashim Mohamed.

Source:-Itv

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad