Amisi Tambwe akikimbia kushangilia baada ya kuifungia bao pekee Yanga SC dhidi ya Khartoum N ya Sudan leo Julai 26,2015.
YANGA
SC itamenyana na Azam FC katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Hiyo
inafuatia ushindi wa bao 1-0 jioni ya leo dhidi ya Khartoum N ya Sudan
katika mchezo wa mwisho wa Kundi A Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na
kwa matokeo hayo, Yanga SC inamaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi
hilo kwa pointi zake tisa, baada ya kushinda mechi tatu, zikiwemo dhidi
ya KMKM ya Zanzibar 2-0 na Telecom ya Djibouti 3-0.
Bao
hilo pekee la Yanga SC leo limefungwa na mshambuliaji wake wa kimataifa
wa Burundi, Amisi Joselyn Tambwe dakika ya 30 akimalizia kwa kichwa
kona iliyochongwa na Nahodha Haruna Niyonzima kutoka Rwanda dakika ya
30.
Sifa
za kipekee zimuendee kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ aliyeokoa michomo
mingi ya hatari langoni mwake hadi Yanga SC kuulinda ushindi huo.
Safu
ya ulinzi ya Khartoum yenye mabeki warefu ilikuwa kikwazo cha
mashambulizi ya mipira mirefu kutoka pembeni ya Yanga, kwani waliicheza
kwa wingi na kuiondosha katika hatari.
Yanga
SC inamaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Gor Mahia ya Kenya yenye
pointi 10, wakati Khartoum kwa pointi zake saba inamaliza nafasi ya
tatu, ingawa nayo imefuzu Robo Fainali.
Winga wa Yanga SC, Simon Msuva akienda chini baada ya kukwatuliwa na beki wa Khartoum N, Antony Akumu Agay leo. Kulia ni Ahmed Adam. |
Mfungaji wa bao pekee la Yanga SC, Amisi Tambwe akiwatoka mabeki wa Khartoum N |
Beki wa Yanga SC, Joseph Zuttah akimtoka beki wa Khartoum, Wagdi Awad |
Mshambuliaji wa Yanga SC, Malimi Busungu akimtoka beki wa Kahrtoum N, Ahmad Adam |
Robo
Fainali za kwanza zinatarajiwa kuchezwa Jumanne kati ya APR ya Rwanda
na Khartoum N na Gor Mahia na Malakia ya Sudan Kusini, wakati za pili
zitachezwa Jumatano kati ya Al Shandy ya Sudan na KCCA ya Uganda na
baadaye, Yanga SC na Azam FC zote za Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment