Pichani:
Kati ya makundi matano yaliyopita kwenye usaili wa kwanza wa Dance 100% (2015)
- Temeke. Kundi linaitwa 'The Best Boys Kaka Zao'.
Usili wa
kwanza wa Dance 100% (2015) umefanyika kwa mafanikio makubwa Temeke jijini Dar
es Salaam, ambapo makundi ya Team ya Shamba, The WT Group, WD, The Best Boys
Kaka Zao na Team Makorokocho wameweza kushinda nafasi ya kuingia katika
michuano kutoka wilaya ya Temeke.
Makundi haya
yamechuana vikali na mengine 6 yanayokamilisha idadi ya makundi 11, UNI 6 Crew,
GMF Crew, TWC, Dar Crew, Noma Sana Crew, na Viga Stars yaliyojitokeza kuwania
nafasi hiyo katika usajili huo wa kwanza.
Mratibu wa
mashindano hayo kutoka East Africa Television na East Africa Radio, Bi Happy
Shame, amesema kuwa amefurahishwa na utulivu na amani ambayo wapenda burudani
Temeke wameonyesha leo, huku pia kukiwa na vipaji mbalimbali kutoka makundi
yaliyojitokeza katika usaili huo wa kwanza.
Akizungumza
baada ya kumalizika michuano ya usaili huo, mratibu wa Dance 100% kutoka
BASATA, Kwerugira Maregesi, mbali na kufurahishwa na vipaji vilivyojitokeza,
amekumbushia umuhimu wa makundi hususan yale yanayotarajiwa kushiriki usajili
unaofuata, kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa kujiwezesha kushinda,
ikiwepo ubunifu katika mitindo ya kudansi, kuburudisha na muonekano, huku
akishauri kupunguzwa kwa mitindo ya sarakasi na kuongezwa ladha katika upande
wa dansi zaidi.
Majaji Super
Nyamwela, Queen Darleen na Shetta wametumia umakini nkubwa kuhakikisha wanatoa
alama zinazostahili kwa mujibu wa vigezo kwa washiriki wote, huku burudani
mbalimbali zikijiri zikishereheshwa kikamilifu na watangazaji rasmi wa Dance
100 kwa mwaka huu, T-Bway 360 na mrembo Maggie Vampire.
Majaji pia
kila mmoja kwa nafasi yake wametaka washiriki watakaoendelea kujitokeza
kujipanga zaidi wakizingatia vigezo vilivyowekwa, ambavyo ndivyo wanavyovitumia
kutoa maksi (alama) zitakazowawezesha kufikia ushindi.
Usajili wa
pili wa mashindano haya makubwa kabisa ya kudansi utafanyika katika viwanja vya
Don Bosco Upanga siku ya Jumamosi Tarehe 01 Agosti 2015, ambapo makundi mengine
matano yatasakwa kushiriki katika michuano hiyo kwa mwaka huu.
Usikose kujionea
kwa urefu yote yaliyojiri pale TCC
Chang'ombe katika mashindano ya usajili huo, kwa kutazama ting'a namba moja kwa
vijana EATV, siku ya Jumamosi, kuanzia saa 12 na nusu jioni.
East Africa
Television na East Africa Radio inaleta Dance 100% kwa kupewa nguvu na mtandao
wa Vodacom Tanzania na Coca Cola ambao ndio kinywaji rasmi cha dance 100%
(2015). |
No comments:
Post a Comment