KURA ZA MAONI CHADEMA / CCM 2015:-Fahamu Matokeo yake kwa Wabunge wengi CCM, CHADEMA watetea nafasi zao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 26, 2015

KURA ZA MAONI CHADEMA / CCM 2015:-Fahamu Matokeo yake kwa Wabunge wengi CCM, CHADEMA watetea nafasi zao.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amepita bila kupingwa katika mchakato wa kura ya maoni ya ubunge wa jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro, baada ya kuvuna kura 269.

Licha ya kupita kwa kishindo,  wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi huo, walimpigia Mbowe kura tano za kumkataa.





GEITA: VICK KAMATA  ATETEA VITI MAALUM
VICK Kamata, amefanikiwa kutetea nafasi yake ya ubunge wa Viti maalum kupitia CCM Mkoa wa Geita, baada ya kuongoza katika kura za maoni kwa kupata kura 426 na kuafuatiwa na Josephine Chagula aliyepata kura 419.

ARUSHA: CATHERINE MAGIGE APETA
 
 Mbunge  wa Viti Maalum Vijana (UVCCM), Catherine Magige, ameibuka kidedea kupitia viti maalum Jumuiya ya Wanawake CCM Mkoa wa Arusha (UWT), kwa kupata kura 409 kati ya kura 560 zilizopigwa huku kura tatu zikiharibika. Mshindi wa pili katika matokeo hayo ni Vailet Mfuko aliyepata kura 248, kati ya kura hizo zilizopigwa kumtafuta mwakilishi wa pili.

AMINA MOLEL ASHINDA
 
Kundi la watu wenye ulemavu:  Amina Mollel alishinda kwa kuzoa kura 362 na kumbwaga mwenzake katika kundi la walemavu Christina Manyenye aliyepata kura (196).

TUMWAGILE MWAKYUSA: KUNDI LA WASOMI
 
Kundi la wasomi: kuwa ni Tumwagile Mwakyusa alipata kura (502) na kumbwaga mwenzake Jesca Njau (51) Nafasi ya kundi la mashirika yasiyo ya kiserikali inawaniwa na Anjela Bayo ambaye hakuwa na mpinzani alipata kura zote 560.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chadema, Lazaro Massay, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, amebwagwa katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti cha ubunge katika kura za moani zilizopigwa juzi.

Alibwagwa na mgombea mwenzake Willy Qhambalo. Qhambalo alishinda kwa kura 217 kati ya kura 302 ambapo mpinzani wake wa karibu Massay alipata kura 81.

MOROGORO: WABUNGE MSAFIRI, ISHENGOMA, SARA WAULA
 
Wabunge watatu wa Viti Maalumu Sara Msafiri, Dk. Christine Ishengoma na Magreth Mkanga wamefanikiwa kuzitetea tena nafasi zao.

Wabunge hao wamepita kwenye  uchaguzi wa kura za maoni wa Umoja wa Wanawake (UWT) kupitia mkoa wa Morogoro.

Dk.  Ishengoma alishinda kwa kura 641 kati ya 771 zilizopigwa. Msafiri alichanguliwa kwa kura 608.

Kwa upande wa vyuo vikuu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe , Dk. Jasmine Bunga, ameshindwa nafasi ya kwanza kwa kupata kura 310.

Katika kinyang’anyiro cha ubunge Viti Maalumu kwa watu wenye ulemavu,  mchuano ulikuwa mkali kati ya mtetezi wa kiti hicho Margaret Mkanga ambaye alipata kuwa 424 kati ya 759 zilizopigwa.

Muingizaji wa filamu nchini Wastara Issa, alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 252.

Kundi la Ubunge Viti Maalumu kupitia NGO’s , Christina Kulunge alishinda kwa kura 225.

Kundi la wafanyakazi, mgombea aliyejitokeza alikuwa Mhandisi Vidate Ligalama ambaye alipigiwa kura ya ndiyo kwa kupata kura 651 na 26 za hapana.

DODOMA: Mbunge wa Viti Maalumu, Felister Bura (CCM) amefanikiwa kutetea kiti hicho baada kushinda kura 457. Mshindi wa pili ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Fatuma Toufiq aliyepata kura 368.

Shamsa Mangunga aliambulia kura 25 kati ya kura 728. Hata hivyo uchaguzi huo umedaiwa kugubikwa na vitendo vya rushwa hali iliyosababisha wagombea 19 kati ya 22 kususia kusaini matokeo ya uchaguzi huo.

Kupitia kundi la watu wenye ulemavu, msanii wa muziki wa kizazi kipya Khadija Shaaban maarufu Keisha, aliibuka mshindi kwa kupata kura 340.

Kundi la wasomi aliyeshinda ni Juliana Manyerere, kundi la Asasi zisizo za kiserikali aliibuka Chiku Mugo huku katika kundi la wafanyakazi Mwalimu wa shule ya Msingi Kizota Mwanamanga Mwanduga akishinda nafasi hiyo.

Mmoja wa wagombea hao, Judith Mieya alisema amegomea kusaini matokeo kutokana na kushindwa kukubaliana na hali ya utovu wa nidhamu katika chama chao.

MBEYA:  HILDA NGOYE AANGUKA VIBAYA
 
Mbunge mkongwe wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Hilda Ngoye kupitia CCM, amekuwa mbunge wa kwanza mkoani hapa kupoteza nafasi yake baada ya kuagushwa vibaya kwenye uchaguzi uliofanyika jana jijini Mbeya.

Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Mary Mwanjelwa, aliibuka kidedea kwa kura 505 na kuwabwaga wagombea wenzake 11.

Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya, Mwangi Kundya alisema kuwa kura zilizopigwa zilikuwa 625, kura mbili ziliharibika na kura halali zilikuwa 623.

Aliyemfuata ni Mary Obadia aliyepata kura 192 huku Ngoye akishika nafasi ya tatu kwa kuambulia kura 164.

WABUNGE MBEYA WATETEA NAFASI ZAO
 
Wabunge wengine wanaoendelea kutetea nafasi zao mkoani Mbeya ni Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela), Dk. Ariko Kibona (Ileje), Godfrey Zambi (Vwawa), Mchungaji Luckson Mwanjale (Mbeya Vijijini), Philip Mulugo (Songwe), Victor Mwambalaswa (Lupa) na Dickson Kilufi (Mbarali) wote kupitia CCM, David Silinde (Momba) na Joseph Mbilinyi Maarufu kwa jina la Mr. II Sugu (Mbeya Mjini) kupitia Chadema).

SONGEA: Joseph Fuime ambaye alikuwa diwani wa kata ya Songea Mjini ameibuka mshindi kwa kupata kura 139 kati ya kura 214 zilizopigwa katika kura za maoni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 
 *Taarifa hii imeandaliwa na John Ngunge, Cynthia Mwilolezi, Arusha, Ashton Balaigwa (Morogoro), Emmanuel Lengwa (Mbeya), Gideon Mwakanosya (Songea), Jacqueline Massano, Agusta Njonji (Dodoma), Godfrey Mushi (Kilimanjaro)

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI 


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad