KAGAME CUP 2015:- Azam FC sasa rasmi fainali Jumapili Agosti 02,2015 na Gor Mahia ya Kenya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 31, 2015

KAGAME CUP 2015:- Azam FC sasa rasmi fainali Jumapili Agosti 02,2015 na Gor Mahia ya Kenya.


Mfungaji wa goli la Azam FC Shah Farid Mussa (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake wa Azam mara baada ya kuigungia timu yake goli lililoivusha mpaka hatua ya fainali.

 Azam FC ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya Kagame Cup wafanikiwa kutinga fainali ya mashindano hayo mara ya pili sasa, baada ya kuilaza KCCA ya Uanda kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa nsu fainali uliomalizika jioni ya leo July 31,2015 kwenye dimba la Taifa.


Goli pekee la Azam limefungwa na Shah Farid Mussa dakika ya 76 kipindi cha pili na kuihakikishia Azam kucheza fainali ya Kagame kwa mwaka 2015,  baada ya awali, mwaka 2012 kufungwa na Yanga SC 2 - 0 Dar es Salaam pia.


Mabingwa wa kenya-Gor Mahia.

Michuano hiyo sasa ya CECAFA Kagame Cup 2015 inazidi kushika kasi katika ardhi ya jiji la Dar es salaam, na kwamba timu ambazo zimefika kwenye hatua hii zinastahili kupewa heshima kwani haikuwa kazi nyepesi kuvuka huko nyuma waliokotoka.

 Mabingwa wa Kenya ni miongoni mwa timu ambayo inazungumziwa sana na wanasoka mbalimbali hasa kutokana na soka wanaloonesha pamoja na kumailza vizuri kwenye makundi huku pia wakifanya vyema kwenye hatua ya robo fainali.

Leo wameshinda magoli 3-1 dhidi ya Al Khartoum , kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa leo July 31, 2015,saa 7:30 mchana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kutinga fainali ya kombe la Kagame 2015 .

Wachezaji wa Gor Mahia wakiwa wanacheza kushangilia goli lao la pili lililofungwa na Innocent Wafula kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kagame.

Mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya Michael Olunga akijaribu kuchukua mpira mbele ya mlinzi wa Khartoum.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad