UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:-NEC yaanza kutoa fomu ya Urais ,Ubunge pamoja na Udiwani kesho na kumalizika kwa zoezi la utoaji fomu hizo ni Agosti,21 , 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 31, 2015

UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:-NEC yaanza kutoa fomu ya Urais ,Ubunge pamoja na Udiwani kesho na kumalizika kwa zoezi la utoaji fomu hizo ni Agosti,21 , 2015.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva (katikati) akizungumza na waandishi habari juu  ya maendeleo mbalimbali katika kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo July 31,2015 Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam,Kulia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji Uchaguzi,Clothilde Komba.



TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kuanza kutoa fomu ya urais ,Ubunge pamoja na Udiwani kesho Jumamosi Agosti 01,2015 na kumalizika kwa zoezi la utoaji fomu hizo ni Agasti,21 mwaka huu,2015.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,July 31, 2015 jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu,Damian Lubuva  amesema wakati wa uchukuaji wa fomu ya urais itatolewa bure lakini wakati wa kurudisha anatakiwa kuweka dhamana ya Sh.milioni Moja na wadhamini 200 katika kila mkoa na kuwepo kwa mikoa miwili Zanzibar.

Jaji Lubuva  amesema kuwa wakati wa kuchukua fomu viongozi wa vyama vya kisiasa wanatakiwa kuchukua fomu na kurudisha bila kuwa na kundi kubwa ambalo linaweza kusimamisha shughuli za watu wengine.

Amesema kwa fomu za ubunge ni sh.50,000  na udiwani sh.5000 ambapo wanatakiwa kuchukulia katika ofisi za wilaya na uchukuaji huo lazima uwe wa kistaarabu katika kuweza watu wengine waendelee na shughuli zao.

Lubuva amesema kuwa  wanasiasa wanatakiwa  na lugha za kistaarabu katika mikutano yao katika kujenga demokrasia iliyo ya ukweli.

Hata hivyo amesema kuna baadhi ya vijana wanauza kadi za tume ya taifa ya uchaguzi na kutaka vyombo vya usalama kuchunguza pamoja na kuwachukulia hatua watu wanaouza kadi hizo. 
Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akizungumza na waandishi habari juu   jeshi la polisi lilivyojipanga katika suala la ulinzi kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari wakifatilia wa taarifa ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo July 31, 2015 Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kuwa uchaguzi unaendana  na usalama hivyo jeshi limejipanga katika ulinzi katika kipindi hiki.

Kova amesema kuwa Jeshi litaendelea kushirikiana na viongozi wa siasa katika kuleta amani katika kipindi cha uchaguzi.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad