AJALI / PICHA :-Watu wanne wamefariki katika ajali ya Treni Morogoro Leo Julai 01,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 01, 2015

AJALI / PICHA :-Watu wanne wamefariki katika ajali ya Treni Morogoro Leo Julai 01,2015.

Watu wanne wamefariki dunia na 21 kujeruhiwa baada ya basi aina ya Isuzu kugonga treni ya abiria iendayo bara katika kilomita 276/0 kati ya Stesheni za Kimamba na Kilosa mkoani Morogoro saa 11:25 asubuhi leo Julai 01, 2015. 

Wahanga walipakiwa katika treni hiyo na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.

Basi lilohusika ni lenye namba za usajili T837CTM Isuzu Coaster linalomilikiwa na Feisal A. Khuwel wa Kilosa.

Taarifa kutoka eneo la tukio limefafanua kuwa waliofariki ni wanaume wawili, mwanamke mmoja na mtoto wa miaka minne. Katika majeruhi 25 wako wanaume 14 na Wanawake 7 na Watano kati yao ni watoto wadogo  ambao wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa!

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ACP Mussa Marambo amefika katika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari kutokuwa mwangalifu wakati akivuka reli na nakuwataka madereva kuwa makini na kuzingatia sheria wanapo vuka katika makutano ya reli na barabara ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima zinazogharimu maisha ya watu.


Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kilosa Dk Denis Haule amekiri kupokea maiti 4 pamoja na majeruhi 25 ambapo kati yao watano hali zao ni mbaya nawamehamishiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi .

 Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad