MAZOEZI SIMBA SC:-Taswira nne za Mazoezi ya Klabu ya Simba SC leo Julai 01,2015 na Kocha wao Muingereza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 01, 2015

MAZOEZI SIMBA SC:-Taswira nne za Mazoezi ya Klabu ya Simba SC leo Julai 01,2015 na Kocha wao Muingereza.

Kocha mpya wa Simba sports club Dylan Kerr leo Julai 01,2015, asubuhi ametambulishwa rasmi kwa wachezaji wa Simba kwenye mazoezi yanayofanyika kwenye viwanja vya Sigara Chang’ombe.

 Wachezaji waliohudhuria mazoezi hayo wameonyesha furaha kubwa kumpata kocha Kerr ambaye ameonesha kuwa ni kocha wa vitendo zaidi, kocha Kerr aliingia uwanjani na kuonesha kwa vitendo mafunzo yake.

Kocha huyo kutoka Nchini Uingereza ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika fani ya mpira wa miguu huku pia akiwa na umahiri wa kufundisha klabu mbalimbali duniani zikiwemo Hai Phong FC Vietnam, Hamilliton Academicals FC na Greennock Morton FC zote kutoka Scotland.

Kocha Kerr pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu za South Africa NFD Nathi Lions FC na  South Africa Thanda Royal Zulu FC kutoka Afrika Kusini.

Kerr ana leseni ya daraja A na B ya ukocha aliyotunukiwa na Shirikisho la soka la Ulaya (UEFA) huku pia akiwa na uzoefu wa utawala katika fani ya michezo.


Katika mazoezi yake ya kwanza kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam, Kerr alionekana yu makini na vitu vingi alipenda kuvitolea mfano kwa vitendo.

Mara kadhaa, kocha huyo alikimbia na wachezaji wake kuonyesha kwamba antaka wafanye vizuri kweli.Picha kwa hisani ya Salehjembe.
 Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad