TANZIA:-Mamia wajitokeza kumzika aliyekuwa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi , EDSON KAMUKARA Kijijini kwao Ihangiro ,Bukoba Vijijini ,Jumatatu June 29, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 30, 2015

TANZIA:-Mamia wajitokeza kumzika aliyekuwa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi , EDSON KAMUKARA Kijijini kwao Ihangiro ,Bukoba Vijijini ,Jumatatu June 29, 2015.

Na Faustine Ruta, Bukoba.

Mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Salvatory Kamukara aliyefariki alhamisi ya wiki iliyopita jijini Dar es Salaam umezikwa Jana June 29,2015  Nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera katika Kijiji cha Ihangiro kitongoji cha Bukujungu na kuagwa na mamia ya waombolezaji.
Marehemu Edson alizaliwa 27,03.1980 na kufariki wiki iliyopita juni 25, 2015 na Marehemu walizaliwa Mapacha na ameacha Pacha mwenzake Edda na  ameacha Mtoto wake anayeitwa Edgar.
Viongozi Dini wakiongoza ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu.
Pacha wa Marehemu Edson (kushoto) Dada Edda na Kulia ni Dada yao Jeniffer kwenye masikitiko makubwa ya Kuondokewa na Ndugu yao.
Katikati ni Dada Joyce akiwa na baadhi ya Wanafamilia.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea(kulia) akifafanua jambo na mhariri Bw. Ansbert Ngurumo kupitia Gazeti la Tanzania Daima. Picha na Faustine Ruta.
Pacha wa Marehemu ( kushoto) kwa machungu akiangalia Picha ya Ndugu yake wakati wa Kumuaga kuelekea nyumba yake ya Milele Jana Jumatatu juni 29, 2015.
V


Dada  wa marehemu Edson Salvatory Kamukara akitoa heshima za mwisho leo jumatatu jioni wakati wa kumuaga.

Kulia ni Mkurugenzi  wa Radio Kasibante Fm 88.5 nae alikuwepo na hapa akitoa salaam zake za mwisho.


Dada yake mkubwa na marehemu Joyce akisoma kwa ufupi historia ya Marehemu Mdogo wake Edson Salvatory Kamukara, Picha na Faustine Ruta.

Mwandishi wa TBC Charles Mwebeya akitoa neno.


Mwandishi mkongwe na mhariri Bw. Ansbert Ngurumo kupitia Gazeti la Tanzania Daima akitoa neno kuhusu msiba huo wa Mhariri Marehemu Edson S. Kamukara Jana Jumatatu June 29,2015 wakati wa Kumuaga rasmi Kijijini kwao Muleba kusini.


Umati mkubwa wa Watu walijitokeza kumuaga

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea akitoa neno kuhusu Msiba huo wa Kijana aliyekuwa Mpiganaji kupitia Kampuni hiyo.

Mwandishi wa TBC Charles Mwebeya akitoa neno kwa Niaba ya waandishi wa Habari Kagera waliojumuika pamoja katika sehemu hiyo kuuaga mwili wa mwenzao Edson Salvatory Kamukara.

Wakati huo huo Mama Mzazi wa Marehemu Edson hakuweza kushiriki alibaki ndani chumbani kwa sababu ya Ugonjwa alionao/ Mlemavu wa Viungo.

Waandishi wa habari Kagera wamejumuika Kuubeba mwili wa Marehemu Edson kuelekea kaburini.

Pacha wa Marehemu akisikitika kuondokewa na mwenzie waliozaliwa pamoja akiwa ni moja ya walioubeba msalaba kuelekea kaburini.
Dada wa marehemu Edson akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Salvatory Kamukara. Picha na Faustine Ruta


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad