UCHAGUZI WA WABUNGE BURUNDI:-Mtazame Rais Nkurunziza alivyowasili na Baiskeli kupiga kura. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 30, 2015

UCHAGUZI WA WABUNGE BURUNDI:-Mtazame Rais Nkurunziza alivyowasili na Baiskeli kupiga kura.

Rais wa Burundi,Bw. Pierre Nkurunziza akiwasili kwenye kituo cha kupiga kura kwa usafiri wa baiskeli hapo jana June 29, 2015.
Rais Nkurunziza akiwa kwenye foleni kwenda kupiga kura yake ya kumchagua mbunge.
Rais Nkurunziza akipiga kura yake.

RAIS wa Burundi, Pierre Nkurunziza Jana June 29, 2015  amepiga kura katika eneo la Ngozi kwa ajili ya kumchagua mbunge wa Jimbo lake.

Nkurunziza amewasili katika kituo cha kupigia kura akitumia usafiri wa baiskeli akiwa amesindikizwa na wapambe wake.
Baadaye rais huyo anayetaka kuwania URAIS  kwa muhula wa tatu alijipanga kwenye foleni ili apige kura huku pembeni yake wakiwepo walinzi wake.

Aidha uchaguzi  wa wabunge unaendelea nchini Burundi licha ya maandamano na ghasia dhidi ya uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa kutaka kuwania muhula wa tatu.

Upinzani umesusia uchaguzi huo huku Muungano wa Ulaya ukieleza kuwa uchaguzi huo utazidisha mgogoro uliopo.

Umoja wa Afrika (AU) umekataa kutoa waangalizi ukisema kuwa baadhi ya masharti yaliowekwa hayajaafikiwa kwa uchaguzi kuwa huru na haki.

Zaidi ya watu 70 wameuawa tangu mgogoro huo uanze huku takribani watu 130,000 wakilitoroka taifa hilo.


Picha na BBC

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad