“Tanzania ni
moja ya nchi zilizofanya vizuri katika kuhama kutoka kwenye mfumo wa habari wa
analogia kwenda digiti kwa ubora wa hali ya juu hivyo kuzinduliwa kwa Studio za
Azam TV kutaendeleza kuongeza ufanisi wa ubora wake,”Amesema Rais Kikwete.
Amesema
sekta ya habari ni moja ya mhimili mkubwa hapa nchini ambao kazi yake ni
kuhakikisha kuwa suala la Demokrasia linaendelea kukua na kuthaminiwa, hivyo
Serikali itaendelea kusimamia uhuru wa vyombo vya habari kwa kutunga sheria
zisizo kandamizi.
Amesema
ubora wa vipindi, teknolojia sahihi na waandishi na watangazaji wenye weledi
mkubwa utakuwa chachu katika kuifanya Azam tv iweze kutoa bidhaa bora hivyo
kuongeza ushindani .
Aidha
amesema uwekezaji wa ndani kwa Mtanzania unaleta heshima kwa Taifa la Tanzania
ikiwa ni pamoja na kuongeza pato la mtanzania na kupunguza adha ya ajira
inayoendelea kukua kila siku nchini.
"Siku
zote penye bidii penye maarifa penye mipango ya uhakika hakuna kisichowezekana,
hawa jamaa wameanzia mbali sana bidiii imewafanya wafikie mahali hapa walipo:-
aliongeza, Tumezoe kula vitu vya Azam, kunywa vitu vya Azam, kushabikia timu ya
Azam na sasa tutasikiliza Azam, hii ni kazi nzuri kwa taifa hili alipongeza
Rais Kikwete"
Amesema
kampuni ya Said Salim Bhakres (SSB) ni moja ya kampuni inayoongoza kwa kutoa
ajira mbalimbali kwa watanzania hapa nchini, pia wanaongoza katika kulipa kodi
stahiki za mapato hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kasi.
Aidha Rais
Kikwete amewataka wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kuendelea kusimamia sera ya
ubora wa bidhaa, hivyo hata kwenye bidhaa ya utangazaji wajikite katika suala
hilo la ubora.
|
No comments:
Post a Comment