HABARI / PICHA :-Ni za Athari ya Mvua ya mawe wilayani Kahama March 03,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 06, 2015

HABARI / PICHA :-Ni za Athari ya Mvua ya mawe wilayani Kahama March 03,2015.

Moja ya nyumba zaidi ya  160 ikionekana kuharibika vibaya huku pia nyingine kuanguka na kuezuliwa paa kutokana na upepo mkali na watu wengine zaidi ya 900 wameripotiwa kukosa makazi katika Kijiji cha Mwakata,kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyang’a baada ya  kubomoka kutokana na mvua ya mawe iliyonyesha kijijini hapo March 3, 2015. 




Mpaka jana March 05,2015, idadi ya watu waliopoteza maisha katika maafa hayo yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha ikiambatana mawe, upepo mkali na kubomoa nyumba za wananchi Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, ikiongezeka kutoka 42 na kufikia 46, baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamelihusisha janga hilo na ushirikina.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Mwakata wilayani Kahama, Salum Mohamed,alimweleza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa baadhi ya wananchi wamejenga dhana kuwa tukio hilo limetokana na ushirikina.

Hata hivyo, Pinda aliyewasili hapa jana, aliwataka wananchi hao kuachana na dhana hiyo potofu kuwa mvua zilizonyesha na kusababisha maafa hayo, zimetokana na ushirikina.

Mvua hiyo ilinyesha juzi March 03,2015 usiku na kuleta maafa katika vijiji vya Mwakata, Nyumbi na Magung’hwa vilivyopo kata ya Isaka wilayani Kahama.

Idadi hiyo imeongezeka kufuatia majeruhi wanne waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kufariki dunia usiku wa kuamkia jana kuongeza idadi  ya waliokufa katika janga hilo kufikia 46.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI





Moja ya nyumba zaidi ya  160 ikionekana kuharibika vibaya katika Kijiji cha Mwakata,kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyang’a baada ya  kubomoka kutokana na mvua ya mawe iliyonyesha kijijini hapo March 6, 2015. 



Mifugo nayo iliathiriwa na mvua hiyo kwa Kufa  katika Kijiji cha Mwakata,kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyang’a baada ya  mvua ya mawe iliyonyesha kijijini hapo March 6, 2015. 


UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad