UHURU WA HABARI:-JK akana kuyumbishwa na kashfa za Ufisadi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 07, 2015

UHURU WA HABARI:-JK akana kuyumbishwa na kashfa za Ufisadi.

Rais Jakaya Kikwete akiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa kituo cha televisheni cha Azam TV, Tido Mhando (kushoto)na msimamizi wa vipindi, Yahya Mohamed wakati wa uzinduzi wa studio za televisheni hiyo jijini Dar es Salaam jana March 06, 2015. Picha na Emmanuel Herman.

Rais Jakaya Kikwete amesema haoni tatizo kwa vyombo vya habari kuandika kashfa zinazoibua mijadala kwenye jamii kwa kuwa yanasaidia uongozi kujirekebisha, lakini akaonya kuwa vyombo hivyo  vikitumia uhuru wao kuchochea chuki, vurugu na mifarakano, Serikali haitavumilia.

Rais Kikwete alikuwa akijibu swali kutoka kwa Tido Mhando wa Azam Media kuwa, anajisikiaje pale vyombo vya habari vinapoibua kashfa nzito kama za uchotwaji fedha kwenye akaunti ya escrow na mkataba wa uzalishaji umeme wa Richmond ambazo alisema zilionekana kutikisa Serikali.

Tido alimuuliza swali hilo wakati wa mahojiano maalumu kwenye hafla ya uzinduzi wa studio za kituo cha televisheni cha Azam TV jana March 06,2015.

Sioni tatizo,” alisema Rais Kikwete kwenye mahojiano hayo.

Alisema hachukizwi na habari hizo na hana tatizo na vyombo vya habari, kwani kwa namna moja au nyingine zinasaidia Serikali yake kujiimarisha na kufanya kazi kwa weledi zaidi.

Ukiandika masuala ya uchochezi, lazima tutakuchukulia hatua, lakini mkiandika kuikosoa CCM, hilo sina shida nalo,” alisema Rais Kikwete.

Licha ya kauli hiyo, Rais Kikwete alisisitiza  kuwa, “Tunatakiwa tuwe na uhuru unaozingatia weledi katika utendaji wa kazi …Serikali haiwezi kuvumilia kuona baadhi ya vyombo vya habari vinatumia uhuru huo kuchochea chuki, vurugu na mifarakano katika nchi.”

Uzinduzi wa studio hizo zilizogharimu Dola 31 milioni za Marekani sawa na Sh55 bilioni za Tanzania, utapanua wigo wa ajira, utafungua ukurasa mpya katika tasnia hiyo na kwamba italeta chachu ya ushindani kwa vyombo vya habari vingine nchini na Afrika.SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA..''


UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad