SEKRETARIETI YA MAADAILI YA VIONGOZI WA UMMA:- Mazito ya Chenge yaibuka. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 26, 2015

SEKRETARIETI YA MAADAILI YA VIONGOZI WA UMMA:- Mazito ya Chenge yaibuka.

Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge  akihojiwa kwenye Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.


Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge ameibuliwa tuhuma nzito kwenye Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma baada ya kudaiwa kuwa aliishawishi kampuni ya Independent Power Solution Limited (IPTL) kuingia mkataba na Tanesco na baadaye kuwa mshauri wa kampuni hiyo binafsi iliyomuingizia Sh1.6 bilioni zinazohusishwa na sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.

Hata hivyo, Chenge, ambaye ni mhitimu wa Shahada ya Umahiri wa Sheria kwenye Chuo Kikuu cha Harvard cha Marekani, aliwasilisha amri ya zuio ya Mahakama Kuu inayokataza chombo chochote cha Serikali kujadili sakata la escrow hadi hapo shauri lililopo mahakamani litakapotolewa uamuzi, jambo lililozua mjadala wa kisheria na kusababisha mwenyekiti wa Baraza la Sekretarieti ya Maadili, Jaji Hamisi Msumi, kuahirisha hadi leo Februari 26,2015.

Chenge ni mmoja wa watu kadhaa wanaotarajiwa kuhojiwa na kamati hiyo kutokana na kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh.306 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa Benki Kuu kwa makubaliano kati ya Tanesco (shirika la umeme la umma) na IPTL baada ya pande hizo mbili kutofautiana kuhusu tozo za malipo ya umeme unaozalishwa na kampuni hiyo binafsi.

Mwingine ni mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Anna Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na ambaye pia aliingiziwa kwenye akaunti yake Sh1.6 bilioni zinazohusishwa na akaunti hiyo ya escrow.

Wote wawili waliingiziwa fedha hizo na James Rugemarila, mkurugenzi wa VIP Engineering iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa za kampuni ya IPTL.

Tuhuma dhidi ya Chenge

Tangu sakata la escrow lianze, haikuwahi kuelezwa kuhusika kwa Chenge kwenye sakata hilo.

Lakini jana, akisoma hati ya malalamiko dhidi ya mbunge huyo wa Bariadi, mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili, Hassan Mayunga alisema mlalamikiwa, akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mwaka 1995, aliishauri Serikali kuingia mkataba wa miaka 20 na IPTL wa kuongeza uzalishaji wa umme.

Mlalamikiwa baada ya kustaafu wadhifa wa AG, Desemba 24 mwaka 2005, mwaka 2006 aliingia mkataba wa kuwa mshauri mwelekezi wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited iliyokuwa inamiliki asilimia 30 ya hisa za IPTL,” alisema Mayunga akikariri hati hiyo ya malalamiko.

“Kitendo cha mlalamikiwa kuingia mkataba na VIP Engineering and Marketing Limited iliyokuwa na asilimia 30 ya hisa kwenye kampuni ya IPTL ni ukiukwaji wa fungu la 6 (j) la Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambalo linamzuia kiongozi wa umma kujinufaisha na utumishi wake uliopita kwa kutumia taarifa alizozipata alipokuwa anatekeleza majukumu yake kwa manufaa binafsi.

“Kitendo cha mlalamikiwa kuendelea kuwa mshauri mwelekezi wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited akiwa na wadhifa wa ubunge ni ukiukwaji wa fungu la 6(e) la Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambalo linamzuia kiongozi wa umma kujiingiza katika mgongano wa maslahi.”

Mwanasheria huyo aliendelea kusema kuwa mkataba ambao mlalamikiwa aliingia na kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited ulimpatia manufaa ya kifedha ya Sh1.617 bilioni kinyume na fungu la 12(1)(e) la Sheria ya maadili ya viongozi wa umma. Aliongeza kuwa mlalamikiwa hakutamka maslahi aliyokuwa nayo katika mkataba wa Tanesco na IPTL kinyume na fungu 14 la sheria ya Maadili.SOMA ZAIDI HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA.


UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad