![]() |
|
Wakati CCM
ikisubiri Februari 2015, kufanya tathmini kuona kama baadhi ya wagombea wake wa
urais wametekeleza masharti ya adhabu zao, washindani wao wa Ukawa, Jumanne
ijayo ya Januari 19,2015 watakutana kujadili mambo mbalimbali, ukiwamo mchakato
wa kuwapata wagombea wake wa urais, ubunge na udiwani, imefahamika.
Tangu mwaka
huu 2015, uanze zimekuwapo pilikapilika nyingi za kisiasa ndani ya vyama vya
siasa na Jumanne iliyopita CCM ilifanya kikao cha Kamati Kuu mjini Zanzibar na
kutoa maazimio yanayogusia mchakato huo lakini ikasita kutaja ratiba rasmi ya
mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM.
Wakati hali
ikiwa hivyo, habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya viongozi wa
Ukawa, umoja huo utakutana jijini Dar es Salaam Januari 20,2015 ukiwa na ajenda
mbalimbali kuhusu ushirikiano wao, likiwamo suala la kupata wagombea huku vikao
vya ndani ya vyama vikitarajiwa mwishoni mwa mwezi huu.
Mwenyekiti
Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alithibitisha jana kuwapo kwa kikao hicho Jumanne
akisema kutakuwa na ajenda nyingine lakini: “Suala la kupata wagombea nalo
huenda likajadiliwa. Kuhusu suala la mgombea urais wa Ukawa, linaweza kuwa
sehemu ya mazungumzo lakini halipo kwenye ajenda.”
Ajenda
nyingine alizotaja ni mwongozo wa Ukawa, kura ya maoni ya Katiba, changamoto za
uandikishaji wa daftari la wapigakura, hali ya uchumi na tathmini ya Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa uliomalizika Desemba mwaka jana 2014.
Mbatia, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi alisema watajadili ajenda hizo ili kuhakikisha
wanatafuta majibu ya changamoto zilizopo kwa sasa.
Kiongozi
huyo pia alithibitisha taarifa kuwa kila chama ndani ya Ukawa kupitia vikao
vyake kitateua majina ya wagombea ambao watashindanishwa ndani ya umoja huo,
akisema kabla ya Machi, jina la mgombea urais ndani ya chama chake litakuwa
limeshapendekezwa.
Awali,
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema vikao vya chama hicho
vinavyotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu vitakuwa na ajenda ya uchaguzi
vitakavyojadili mwelekeo wa uchaguzi huo kama kalenda yake inavyosema.
Nyambabe
alisema kamati hiyo imekuwa ikifanya kazi, ikijumuisha wajumbe wasiopungua
watatu kutoka kila chama ili kufanya tathimini, kuchambua na kuratibu shughuli
zote za uchaguzi.
Kuhusu
kupata mwongozo wa Ukawa, Nyambabe alisema: “Namna ya kupata mgombea, ilani
moja na mwelekeo, vinaweza kuonekana kuanzia Februari baada ya vyama kukaa
vikao vyake.”
Wakati
Nyambabe akisema hayo, kumekuwa na taarifa katika vyombo vya habari kuwa CUF
kimeshatangaza kumsimamisha Profesa Ibrahim Lipumba kuwania urais, ambazo hata
hivyo, zimekanushwa na Naibu Katibu Mkuu wake Bara, Magdalena Sakaya.GONGA HAPA KUSOMA ZAIDI
|
Friday, January 16, 2015
Home
SIASA
UCHAGUZI MKUU TANZANIA:- mwanzo Habari Kitaifa Kitaifa Urais 2015.......UKAWA waanza safari....''
UCHAGUZI MKUU TANZANIA:- mwanzo Habari Kitaifa Kitaifa Urais 2015.......UKAWA waanza safari....''
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment