![]() |
|
Mabaki ya nyumba
ya mzee ambayo ilichomwa kutokana na imani za kishirikina. Picha na
Maktaba .
Madai ya
kuroga mvua, upigaji ramli, ugomvi ndani ya ndoa, tamaa ya kurithi mali, ardhi
na ng’ombe ni miongoni mwa mambo yanayoelezwa kusababisha ongezeko la mauaji ya
wazee vikongwe katika baadhi ya mikoa nchini Tanzania.
Shirika
linalojishughulisha na haki za wazee la Help Age International, limetaja sababu
hizo kuwa ndizo zilizoendeleza wimbi la mauaji hadi kufikia idadi ya wazee
zaidi ya 4,612 kuuawa kutoka mwaka 1998 mpaka 2014.
Anasema kwa
mujibu wa ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ya mwaka 2009,
wanawake wazee 2,583 waliuawa katika mikoa minane ikiwa ni wastani wa mauaji
517 kila mwaka.
“Takwimu za
Mkoa wa Mwanza pekee, ambao ndiyo ulikuwa na mauaji mengi nchini zilionyesha
kuwa wanawake wazee 689 waliuawa kati ya mwaka 2002 na 2007 ikiwa ni wastani wa
mauaji 140 kila mwaka,” anasema Meneja wa Programu wa Help Age, Flavian
Bifandimu.
Anasema
taarifa kutoka Shinyanga pia zinatisha, kwani wanawake wazee 242 waliuawa kati
ya Januari 2010 na Juni 2011.
Sababu za Mauaji.
Mwenyekiti
Mtendaji kutoka asasi ya Maperele ya Magu, Joseph Mandalo anasema mauaji ya
wazee Mwanza na maeneo yanayouzunguka mkoa, yalitokana na ugomvi wa kifamilia
na ndoa.
“Mauaji ya
wazee yana sababu nyingi, mara nyingi yanaanzia katika migogoro ya familia na
tatizo kubwa ni ardhi na mali. Sasa inapofikia hatua wanazihitaji, wanatumia
kigezo cha kwamba ni mchawi ili wapate kirahisi,” anasema Mandalo.
Anaongeza:
“Wengi wanatumia njia za mkato kujipatia mali kwa kuondoa uhai wa wengine.
Ukichunguza kwa umakini utagundua kwamba mipango ya mauaji inafanywa na
wanafamilia.’’
Mwenyekiti
wa chama cha watu wanaoishi na Ukimwi Wilaya ya Bukombe, Essau Malifedha
anasema katika mila za Kisukuma, kuna mambo kadhaa kama vile kuchelewa kwa
mvua.
Anasema zinapochelewa jamii humhisi kikongwe
yeyote kuwa ndiye aliyesababisha hali hiyo.
“Usukumani
mvua zinapochelewa kunyesha, wanaamini kwamba ni mwanamke mzee na moja kwa moja
wanakimbilia kupiga ramli. Wakati mwingine ni tamaa za mali, unakuta mzazi
anamrithisha mali mtoto akiwa mdogo, sasa wanapokua wanaona mzee hafi wanaamua
kumuua ili warithi,” anasema Malifedha na kuongeza kuwa mtazamo huo ni athari
itokanayo na ujinga.
Anaongeza
kuwa mauaji kwa wazee yanatofautiana kutoka eneo moja hadi jingine… “Ukiona
shingo imekatwa mara moja unajua ni kabila gani limehusika na mauaji, kama
panga limekata zaidi ya mara mbili ni kabila jingine vivyo hivyo na maeneo ya
mwili na marehemu.”SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA
|
Friday, January 16, 2015
UHALIFU :-Wazee zaidi ya 4,612 wauawa kwa ushirikina Tanzania.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment