|
Mabingwa wa
Italia, Juventus, wakicheza bila ya Nyota wao Carlos Tevez, Andrea Pirlo na
Gigi Buffon, waliopumzishwa wakati Arturo Vidal akiwa mgonjwa, waliifumua
Verona Bao 6-1 kwenye Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Coppa Italiana usiku
wa Jana Januari 15,2015.
Hadi
Mapumziko Juve walikuwa mbele Bao 3-0 kwa Bao mbili za Sebastian Giovinco na
moja la Roberto Pereyra.
Kipindi cha
Pili, Paul Pogba akapiga Bao la 4 na kuifanya Juve iongoze 4-0 lakini Nene
akafunga Bao kwa Verona na Gemu kuwa 4-1.
Alvaro
Morata akaipa Bao la 5 Juve kwenye Dakika ya 63 kwa Penati baada ya Rafael
Marquez kumwangusha Sebastian Giovinco na la 6 kufungwa na Coman.
Juve sasa
wametinga Robo Fainali na watacheza Nyumbani na Parma ambayo iliifunga Cagliari
2-1.
Mechi za
Robo Fainali zitachezwa Februari 4,2015.
Jumanne
Januari 20,2015
2300 AS Roma
vs Empoli
Jumatano
Januari 21,2015
2000
Fiorentina vs Atalanta
2300 Inter
vs Sampdoria
Alhamisi
Januari 22,2015
2300 Napoli
vs Udinese
Robo
Fainali
Jumatano
Februari 4,2015
AC Milan vs
Lazio
Inter/Sampdoria
vs Napoli/Udinese
AS
Roma/Empoli vs Fiorentina/Atalanta
Juventus vs
Parma
Nusu
Fainali
Machi 4
& Aprili 8,2015
AC
Milan/Lazio vs Inter/Napoli/Sampdoria/Udinese
AS
Roma/Fiorentina/Empoli/Atalanta vs Juventus/Parma
Fainali
Juni 7,2015-
Rome
|
No comments:
Post a Comment