MAPINDUZI CUP 2015:- Fainali ni Simba SC Vs Mtibwa Sugar Jumanne Januari 13,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 11, 2015

MAPINDUZI CUP 2015:- Fainali ni Simba SC Vs Mtibwa Sugar Jumanne Januari 13,2015.

Kocha Goran Kopunovic  anasema kikosi chake kitaendelea kupambana kwa kila hali ili kishinde mechi yao ya fainali dhidi ya Mtibwa Sugar.


Fainali ya Kombe la Mapinduzi inapigwa Jumanne Januari 13,2015 kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Simba na Mtibwa Sugar zimetinga hatua hiyo ya Fainali ya Mapinduzi Cup 2015 baada ya Jana Januari 10,2015 kushinda Mechi zao za Nusu Fainali huko Visiwani Zanzibar.

Simba walitinga Fainali kwa kuichapa Polisi ya Zanzibar Bao 1-0 kwa Bao la Ramadhan Singano.

Nao Mabingwa wa zamani wa Tanzania mara mbili mfululizo, 1999 na 2000, Mtibwa Sugar ya Morogoro wametinga fainali ya michuano ya Mapinduzi mwaka 2015 kufuatia kuitandika JKU ya Zanzibar penalti 4-3.

Mshindi alilazimika kupatikana kwa penalti baada ya timu hizo kushindwa kufungana ndani ya dakika 90.

Fainali hii itachezwa Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar hapo Jumanne Januari 13.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad