EPL 2014/2015:- Matokeo ya mechi za Januari 10,2015 pamoja na Msimamo ulivyo baada ya Liverpool na Chelsea Kushinda. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 11, 2015

EPL 2014/2015:- Matokeo ya mechi za Januari 10,2015 pamoja na Msimamo ulivyo baada ya Liverpool na Chelsea Kushinda.

Pichani ni MENEJA mpya Alan Pardew ameanza vizuri huko Selhurts Park wakati Crystal Palace ilipotoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuitwanga Tottenham Bao 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu Uingereza Jana Januari 10,2015.

 Baada ya Liverpool kufungua pazia la mechi za Ligi kuu Uingereza  kwa ushindi dhidi ya Sunderland kwa ushindi wa taabu wa 1-0 kwa goli la dakika za mwanzoni kabisa Lazar Markovic,Nao Chelsea ambao wanaongoza ligi waliwakaribisha Newcastle United kwenye dimba lao la Stamford Bridge na kupitia wachezaji wao Diego Costa na Oscar walipata magoli 2-0 na yalitosha kuwapa ushindi Chelsea na kuzidi kuimarisha uongozi wao kwenye msimamo wa ligi.
Wakati huo huo wapinzani Mancheste City walisafiri mpaka kwenye uwanja wa Goodison Park kucheza dhidi ya Everton na kuambulia  sare ya 1-1, matokeo ambayo yamewafanya Chelsea waendelee kutanua kwenye msimamo wa ligi.

Jumamosi Januari 10,2015.

Sunderland 0 Liverpool 1   
         
Burnley 2 QPR 1   
           
Chelsea 2 Newcastle 0  
             
Everton 1 Man City 1    
             
Leicester 1 Aston Villa 0   
          
Swansea 1 West Ham 1  
            
West Brom 1 Hull 0    
      
Crystal Palace 2 Tottenham 1   
Ushindi huo umeipeleka Liverpool mpaka nafasi ya 9 Kwenye msimamo wa ligi baada ta kucheza mechi 21 na kupata pointi 32.

Ligi Kuu Uingereza inaendelea Leo ,januari 11,2015 kwa Mechi mbili kati ya Arsenal na Stoke City kisha Man United kucheza na Southampton.

Jumapili Januari 11,2015.

1630 Arsenal v Stoke   
              
1900 Man United v Southampton

MSIMAMO.
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad