AJALI YA MOTO:-Tazama Picha 15 za Lori likiteketea kwa Moto wilayani Ngara mkoani Kagera Januari 11,2015 huku Wananchi wasiowaaminifu wakiiba Mifuro ya Saruji. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 12, 2015

AJALI YA MOTO:-Tazama Picha 15 za Lori likiteketea kwa Moto wilayani Ngara mkoani Kagera Januari 11,2015 huku Wananchi wasiowaaminifu wakiiba Mifuro ya Saruji.

Lori hilo aina ya Scania lenye namba T 178 BEN lililokuwa na tela namba T 382 ADH  lilianza kupata ajali hiyo Jana Januari 11,2015 ,majira ya Saa 12 Jioni katika mteremko mkali wa K9 katika barabara ya Ngara-Burundi lakini Dereva wake ambaye hakupatikana jina lake mara moja  alilimudu ,Ingawa lilimwaga mifuko michache ya Saruji.






Baada ya marekebisho,Lori hilo lilifanikiwa kutoka eneo hilo la mteremko na  kuendelea na safari yake na lilipofika katika mpando wa mlima wa Kumuyange mjini Ngara ndipo lilipowaka moto upande wa kichwa chote kama picha zinavyoonesha.

Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni ubovu wa mfumo wa breki na hakuna kifo wala majeraha.

Jeshi la Polisi wilaya ya Ngara mkoani Kagera limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na linawashikiria Watu kadhaa kwa wizi wa mifuko ya Saruji iliyoibiwa kutoka katika eneo la Ajali.






Pichani ni muonekano wa tela la lori hilo lililokuwa na shehena ya  tani ya Saruji kunusurika kuwaka moto lakini Wananchi wasiowaaminifu kutoka maeneo ya Kumuyange na jirani waliiba Mifuko hiyo na kuliacha kweupe .



UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad