|
Viongozi wa
Ukawa wakizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam. Picha na Emanuel
Herman .
Vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimetangaza rasmi kutoshiriki
katika mchakato wa kura ya maoni ya katiba na kwamba kuanzia sasa vitahamasisha
wananchi kuunga mkono.
Uamuzi huo
umetolewa leo Januari 23,2015 na wenyeviti wa vyama wanaounda umoja huo wa ukawa ambao ni
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD,
Makaidi.
Akizungumza
wakati wa kutoa msimamo huo Profesa Lipumba amesema wamefikia uamuzi wa
kutoshiriki katika zoezi hilo kwa sababu mchakato mzima haukuwa na maridhiano
ya kitaifa.
“Vyama vya
siasa ikiwemo CCM vilikubaliana mwaka jana kwamba zoezi la kura za maoni
lifanyike mwaka 2016 baada ya uchaguzi mkuu, tulisaini wote na Rais Jakaya
Kikwete alikubali, kwa nini mabadiliko yafanyike ghafla” amehoji Profesa
Lipumba.
Amesema
jambo la kushangaza, Rais Kikwete aligeuka na kutangaza kwamba Aprili 30, mwaka
huu kuwa siku ya kupiga kura ya maoni kuhusu Katiba Mpya.
Amesema
pamoja na kutangaza siku ya kupiga kura, bado uandikishaji katika daftari la
wapiga kura haujaanza kwa sababu wanasubiri vifaa.
“Hadi sasa
vifaa vya Biometric Voter Registration (BVR) vilivyopo ni seti 250 wakati vinavyohitajika
ni seti 7500, tume inasubiri hadi sasa, zoezi hili litafanyika kweli?,” alihoji
Lipumba.
“Mbinu hiyo
inafanywa na Serikali kwa sababu Wazanzibari ndiyo wanaona kikwazo kwao,”
alisema Makaidi.
Aprili 16
mwaka jana, Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kutoka vyama vya Chadema, CUF,
NCCR-Mageuzi na NLD walitoka nje wakidai bunge hilo lilikuwa halijadili maoni
ya wananchi yaliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Chanzo:-Mwananchi.
|
No comments:
Post a Comment