![]() |
|
Mfalme Abdulla
enzi za utawala wake.
Mfalme
Abdullah amerithiwa na kakake, Salman, aliye na umri wa miaka 79....Mfalme
Abdullah aliingia uongozini mnamo mwaka 2005 alipomrithi nduguye mwingine,
Fahad.
Hata hivyo tayari alitarajiwa kuwa kiongozi wa Saudia kwa muda wa miaka
kumi kwa sababu mfalme aliyemtangulia alikuwa anaugua kiharusi.
Viongozi
wengi wa dunia wametuma risala za rambi rambi kwa utawala wa Saudia kufuatia
kifo cha mfalme wao Abdullah.
Nchi kama
vile Bahrain na Jordan zimetangaza siku arobaini za maombolezi kwa heshima
yake.
Katibu mkuu
wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon, amempongeza mflame huyo kwa juhudi zake za
kutafuta amani katika mashariki ya kati.
Japo mfalme
Abdullah amesifiwa ndani ya nchi yake na hata baadhi nje ya nchi, wanaharakati
wa haki za binadamu wamejitokeza kukashifu utawala wake wakisema kuwa alileta
mabadiliko machache sana ya kusifika.
Saudi Arabia
ina ushawishi mkubwa katika mataifa ya Pakistan, Bangladesh na India ambapo
inafadhili miradi kadha na shule nyingi zinazotoa mafunzo ya kidini.
Makundi
nchini pakistan kwa muda mrefu yamekuwa yakishutumu baadhi ya shule hizo ambazo
yanasema zinaendesha kampeni za chuki dhidi ya Washia
Chamgamoto
inayomkabili mfalme huyo mpya ni kuhakikisha kuwa msaada wa mamilioni ya ya
dola hauwafikii wale wanaounga mkono chuki.
Makundi ya
haki za binadamu yanaamini kuwa uongozi mpya wa saudi Arabia utatekeleza ahadi
za muda mrefu za kuboresha mazingira kwa mamilioni ya wafanyikazi wahamiaji
kutoka nchi za Asia.
Wanasema
kuwa hadi sasa waajiri nchini Saudi Arabia wana usemi mkubwa juu wa wajiriwa
wao.
Habari Na:-BBC Swahili.
UNGANANASI KATIKA FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Friday, January 23, 2015
BURIANI:-Kwa mfalme wa Saudi Arabia Abdulla.
Tags
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MATUKIO
Labels:
MATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.







No comments:
Post a Comment