|
Gogo akiwa
darasani na wanafunzi wenziwe. …..Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke wa Kenya
ambaye anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita inaaminika ndiye
mwanafunzi mzee zaidi anayesoma shule ya msingi duniani.
Akiwa
ameketi dawati la mbele kabisa darasani ,yuko darasa la tano na amevalia nguo
za shule , Priscilla Gogo Sitienei anamsikiliza mwalimu anayefundisha kwa
makini hukua akiandika majina ya wanyama kwa kiingereza kwenye daftari lake.
Prissilla
alijiunga na shule hii ya 'Leaders Vision Preparatory School' miaka mitano
iliyopita lakini pia aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake cha Ndalat
kilichoko kwenye bonde la ufa kama mkunga miaka sitini na mitano iliyopita.
Darasani
Priscilla anawasaidia wengine wafanye vyema ambao wana umri kati ya miaka 10
hadi 14 na mar azote huwaambia ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo urithi
wao.
Priscilla
anajulikana kama Gogo maana yake bibi katika lugha ya jamii ya
wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa na umri wa miaka 90 katika umri huo
anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo.
Lugha ambayo
Priscilla anajiona yuko huru kuitumia ni lugha mama kwake ki Kalenjin kuliko
kiingereza,pindi anapotakiwa kujieleza kwanini aliamua kujiunga na shule katika
umri wake.
Sababu kubwa
ambayo amekuwa akiitoa,ni ajue kusoma ili amudu kusoma bibilia,lakini pia kwa
umri wake anataka awahamasishe watoto kupata elimu,kwani anawaona watoto wengi
wakiwa hawako shuleni na watoto hao wana watoto.
Gogo apitapo
mitaani haoni shida kukabiliana na watoto ambao hawako shuleni katika muda wa
masomo na kuwauliza kwanini hawako shuleni.
Gogo anasema
watoto hao humjibu kwamba hawaendi shule kwakuwa umri wao ni mkubwa,name
huwaambia mimi ni mkubwa sana kwenu lakini niko shuleni hivyo nanyi jiungeni na
shule.
Kikubwa
kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto wengi waliopoteza muelekeo,wengi wao
hawana baba na wanazurura hovyo mitaani,bila msaada wowote.kutokana na hali
hiyo nataka kuwahamsisha waende shuleni.
Chanzo:-BBC
Swahili.
|
No comments:
Post a Comment