AFCON 2015:-Soma Matokeo ya Mechi za januari 22,2015, Msimamo wa Kundi A & B pamoja na Ratiba ya leo Januari 23. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 23, 2015

AFCON 2015:-Soma Matokeo ya Mechi za januari 22,2015, Msimamo wa Kundi A & B pamoja na Ratiba ya leo Januari 23.

 DR Congo fans arrived in time for the earlier game between Zambia and Tunisia at the same ground .

 Mechi za Pili za Kundi B la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, zimekamilika kwa Sare ya 0-0 kati ya Cape Verde na Congo DR na kuliacha Kundi hilo likiwa wazi kwa yeyote kufuzu ikiwa watapata matokeo mazuri katika Mechi zao za mwiaho.
 

MSIMAMO-KUNDI A.


Mechi hizi zote za Kundi B zilichezwa Januari 22,2015  huko Mjini Ebebiyin Nchini Equatorial Guinea ndani ya Nuevo Estadio de Ebebiyín na mapema Zambia walifungwa Bao 2-1 na Tunisia.

Kwenye Mechi ya mwisho, Zambia wataivaa Cape Verde na Congo DR kucheza na Tunisia.
Katika  Mechi ya pili ya Kundi A la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, Usiku wa januari 21,2015 huko Estadio de Bata Mjini Bata Nchini Equatorial Guinea, Congo wameichapa Gabon Bao 1-0 na kulifunua kabisa Kundi hilo.

Awali hii L, Wenyeji Equatorial Guinea walitoka Sare 0-0 na Burkina Faso na matokeo haya baada ya Mechi mbili kwa kila Timu yamewapa Congo uongozi wakiwa na Pointi 4 wakifuatiwa na Gabon wenye 3, Equatorial Guinea 2 na Burkina Faso 1.

Hali hii inafanya kila Timu iwe na nafasi kutinga Robo Fainali ikiwa matokeo yatawakubali katika Mechi zao za mwisho za Kundi.

Kwenye Mechi hiyo, Congo walipata Bao lao la ushindi katika Dakika ya 48 kutokana na Kona ya Bouka Moutou ambayo ilimaliziwa na Prince Oniangue. 

MSIMAMO-KUNDI A.
Ijumaa Januari 23.

KUNDI C

1900 Ghana v Algeria [Estadio de Mongomo]  

2200 South Africa v Senegal [Estadio de Mongomo]  
           
Jumamosi Januari 24

KUNDI D

1900 Côte d'Ivoire v Mali [Nuevo Estadio de Malabo] 

2200 Cameroon v Guinea [Nuevo Estadio de Malabo]   
        
Jumapili Januari 25

KUNDI A

2100 Gabon v Equatorial Guinea [Estadio de Bata]     
          
2100 Congo v Burkina Faso [Nuevo Estadio de Ebebiyín]  
    
Jumatatu Januari 26

KUNDI B

2100 Congo DR v Tunisia [Estadio de Bata]    
           
2100 Cape Verde Islands v Zambia [Nuevo Estadio de Ebebiyín]  
             
Jumanne Januari 27

KUNDI C

2100 South Africa v Ghana [Estadio de Mongomo]    

2100 Senegal v Algeria [Nuevo Estadio de Malabo]   

Jumatano Januari 28

KUNDI D

2100 Cameroon v Côte d'Ivoire [Nuevo Estadio de Malabo]  
          
2100 Guinea v Mali [Estadio de Mongomo]   


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad